Friday, 13 May 2011

CHADEMA WATIKISA MKOA WA RUVUMA KWA KUFANYA MAANDAMANO MAKUBWA!

Maandamano ya pikipiki yakitembea kutoka maeneo ya Msamara (Hoteli ya Top One Inn) kuelekea viwanja vya shule za msingi vya Kiburang'oma na Mloweka kupitia Barabara ya Peramiho. Maandamano hayo yalitembea zaidi ya kilometa 10 kuelekea Kata ya Lizaboni Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma yaliyoanza saa 9 alasiri leo.





Maandamano yakipita katikati ya mjini wa Songea karibu na Stendi Kuu ya Mabasi yaendayo mikoani.



Kina mama nao hawakuwa nyuma kwa kutembea kilometa 10 kutoka Hoteli ya Top One Inn hapo Msamara walipofikia viongozi mbalimbali wa Chadema kuelekea Lizaboni kupitia barabara ya Peramiho na maadamano hayo yaliishia viwanja vya shule ya msingi ya Kiburang'oma kwa ajili mkutano wa hadhara.






Viongozi mbalimbali wa CHADEMA wakiongoza maandamano wakiwemo M/kiti Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dr. Wilbroad Slaa, Naibu Katibu Zitto Kabwa na wabunge mbalimbali wa chama hicho.


Wakazi wa Manispaa ya Songea na maeneo ya jirani wakifuatilia mkutano wa Chadema katika vya viwanja vya shule ya msingi Kiburang'oma bila kuogopa jua kali.



Wakazi wa Manispaa ya Songea wakifuatilia mkutano wa hadhara kwa makini huku wengine wakifuatilia mkutano huo kupitia  madirisha ya madarasa ya shule ya msingi Kiburang'oma.







Dr. Slaa juu ya gari akisindikizwa na wananchi jioni sana baada ya mkutano kuisha mpaka Hotelini alikofikia kwa maandamano makubwa. Mambo makubwa yaliyozungumziwa katika mkutano huo ni masuara ya Katiba Mpya pamoja na masuala kupanda kwa gharama za maisha n.k. Hata hivyo, Mkoa wa Ruvuma ni wa sita tangu kuanza kwa maandamano yakuzunguka  nchi nzima kwa chama hicho na mkoa wa saba utakuwa ni mkoa wa Iringa.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...