Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Jacqueline Mneney Maleko (wa tatu kushoto) akiongozana na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto) mara baada ya kuwasili katika viwanja vya maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara 'Sabasaba', barabara ya Kilwa, jijini Dar.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (wa pili kushoto) akibadilishana mawazo na Mratibu Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakati wakielekea katika banda la Shirika la Umoja wa Mataifa lilipo Karume Hall mara tu baada ya kuwasili.
Na Modewjiblog team, Sabasaba
Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez, akizungumza na waandishi wa habari alipotembelea banda la Umoja wa Mataifa leo katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara Sabasaba amesema Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa miradi na mikakati ya Umoja wa Mataifa miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki.
Ameongeza kuwa dunia sasa imekuwa kijiji kimoja na Umoja wa Mataifa umekuwepo Tanzania hata kabla ya uhuru, hivyo unakusudia kuendelea kuwepo kushirikiana na watanzania katika kutatua matatizo kwenye Nyanja mbalimbali.