Sunday, 2 August 2015

MTOTO WA MAMA NTILIE JUMAA AWESO ASHINDA KWA KISHINDO UCHAGUZI WA NDANI CCM PANGANI


Ndugu Jumaa Aweso.

Na Mohammed Hammie, Pangani, Tanga

Mtoto wa mama ntilie mwenye uzao halisi kutoka wilayani Pangani mkoani Tanga, Ndugu Jumaa Aweso (pichani) ameibuka na ushindi wa kishindo katika uchaguzi wa ndani wa chama cha mapinduzi CCM.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katibu wa CCM wilayani Pangani Bi Zaina Mlawa amesema kuwa, katika uchaguzi huo uliowashirikisha wagombea wapatao kumi na moja, Ndugu Aweso amekuwa wa kwanza miongoni mwa wagombea hao.

MWAKALEBELA, LUKUVI NA MGIMWA NDANI Y NYUMBA...!



MKUU wa wilaya ya Wanging’ombe, Frederick Mwakalebela ameibuka kidedea katika kura za maoni za kutafuta kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Iringa Mjini kwa kuwabwaga vibaya washindani wenzake 12. (Picha na Friday Simbaya)


Iringa: ZOEZI la kuhesabu kura za kuwania ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kwa majimbo matatu limeendelea vizuri.

Jimbo la Iringa Mjini.

Jimbo la Iringa mjini lilikuwa na wagombea 13 ambao ni Fredrick
Mwakalebela ameshinda kwa kura 40388, Jesca Msambatavangu 2077, Yahaya Msigwa 1097, Augustine Mahiga 745, Mahamood Madenge 423, Addo Mwasongwe ,259, Nuru Hepautwa 191, Frank Kibiki 183, Maiko Mlowe 183, Fales Kibasa171, Kiponda Stephen 135 Mwanilwa Joseph 79 na Adelino Gwilino 66.  Jumla ya kura z zilikuwa 10,216 ,zilizoharibika 220 kura halali 9997.


Jimbo la kalenga

Wagombea ubunge Kwenye Jimbo la kalenga walikuwa watano ambao ni Abbas Kandoro alipata kura 674, Jackson Kiswaga kura 3,439, Brayson Kibasa kura 289, George Mlawa kuwa 301, na Geofrey Mgimwa kura 15550. Jumla zilikuwa kura 22,253 na zilizoharibika zilikuwa kura 32.

DOSARI YAJITOKEZA KURA ZA MAONI UBUNGE JIMBO LA IRINGA MJINI, MGOMBEA ATAKA MCHAKATO USITISHWE


frank Kibiki ambaye pia ni Mwanahabari wa Magazeti ya Uhuru na
Mzalendo wa mkoani 




frank Kibiki akionyesha walivyo kosea jina lake. 



na mwandishi wetu,iringa

WAKATI kura za maoni za kutafuta wagombea ubunge katika majimbo yote nchini kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) zimekipigwa jana, mmoja kati ya wagombea 13 wanaotafuta nafasi hiyo Jimbo la Iringa Mjini, Frank Kibiki anataka zoezi hilo jimboni humo libatilishwe.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...