MKUU wa wilaya ya Wanging’ombe, Frederick Mwakalebela ameibuka kidedea katika kura za maoni za kutafuta kuteuliwa kugombea ubunge jimbo la Iringa Mjini kwa kuwabwaga vibaya washindani wenzake 12. (Picha na Friday Simbaya)
Iringa: ZOEZI la kuhesabu kura za kuwania ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Mkoa wa Iringa kwa majimbo matatu limeendelea vizuri.
Jimbo la Iringa Mjini.
Jimbo la Iringa mjini lilikuwa na wagombea 13 ambao ni Fredrick
Mwakalebela ameshinda kwa kura 40388, Jesca Msambatavangu 2077, Yahaya Msigwa 1097, Augustine Mahiga 745, Mahamood Madenge 423, Addo Mwasongwe ,259, Nuru Hepautwa 191, Frank Kibiki 183, Maiko Mlowe 183, Fales Kibasa171, Kiponda Stephen 135 Mwanilwa Joseph 79 na Adelino Gwilino 66. Jumla ya kura z zilikuwa 10,216 ,zilizoharibika 220 kura halali 9997.
Jimbo la kalenga
Wagombea ubunge Kwenye Jimbo la kalenga walikuwa watano ambao ni Abbas Kandoro alipata kura 674, Jackson Kiswaga kura 3,439, Brayson Kibasa kura 289, George Mlawa kuwa 301, na Geofrey Mgimwa kura 15550. Jumla zilikuwa kura 22,253 na zilizoharibika zilikuwa kura 32.
Jimbo la Ismani
Mbunge wa jimbo la Ismani Willium Lukuvi kwenye kura za maoni alipata kura 10,799, Festo Kiswaga 1237, Hamis Maliga 323,Eliasa Kazikuboma 62, Kiyoyo Antony Sebastian 155, Jumla ya kura zilikuwa 12,560 zilizoharibika zilikuwa kura 42.
Akizungumza katibu wilaya ya Iringa Elisha Mwampashi alisema aliwataka wagombea hao kuwa wamoja kwa ajili ya kukijenga chama huku akisema wagombea hao wasiwabeze wenzake ambao kura hazikutosha kwa sababu bado safari ndefu chama kitaenda kuchuja na kuleta jina la atakaye peperusha bendera ya chama cha mapinduzi jimbo la Iringa amjini.
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Mjini Abeid Kiponza
aliwatakawagombea hao kuacha makundi ndani ya chama ili kuweza kumtafuta mgombea aliye safi.
“Safari hii imeanza tulishapata mgombea urais sasa ni kwenu wabunge na madiwani sitaki kusikia makundi ndani ya chama cha mapinduzi nitakayemsikia anaanzisha kundi nitahakikisha kanuni za chama zitafuatwa juu yake.”alisema Kiponza.
Akizungumza kwa niaba ya wagombea wote wa jimbo la iringa mjini Addo Mwasongwe alisema kuwa maendeleo ya Iringa yanajengwa na wanairinga wenyewe, hata kama hutapata kuleta maendeleo kwa njia ya ubunge tafuta nafasi nyingine utawaletea maendeleo endapo wataungana na kuwa kitu kimoja pasipo kuwa na majungu ndani ya chama.
No comments:
Post a Comment