Mkuu wa Wilaya ya Mufindi (DC) Jamhuri David William ameziagiza halmashauri zote wilayani hapa kuingiza kazi zilizokasimiwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) katika mipango kazi na bajeti.
Alisama kuwa kuna halmashauri hazijaingiza kabisa au zimeingiza kiasa kidogo cha kazi zilizokasimiwa na TFDA katika mipango ya kazi na bajeti.
William alisema hayo jana wakati wa akifunguzua mafunzo ya wakaguzi wa halmashauri na kamati za chakula na dawa kuhusu uimarishaji wa utekelezaji wa majukumu ya TFDA yaliyokasimiwa kwa halmashauri.
Jumla ya wakaguzi 35 na wajumbe 15 wa kamati za chakula na dawa katika halmashauri ya mji wa Mafinga na halmashauri ya Mufindi walipata mafunzo hayo.
Alisema kwamba kutoinzingiza masula ya TFDA katika mipango ya kazi na bajeti kuna kunakwamisha juhudi za serikali katika kudhibiti ubora, usalama na ufanisi wa bidhaa za chakula, dawa, vifaa tiba na vipodozi.
DC William aliziagiza pia halamashauri kutumia fursa ya kanuni mpya ya kukasimu madaraka ya mwaka 2015, ambayo TFDA imeziachia halmshauri zikusanye na zitumie asilimia 100 za makusanyo kwa majengo yale tu yaliyokasimiwa kwa wakurugezi, isipokuwa kwa biashara zile zinazotolewa vibali moja kwa moja na TFDA.
Alisema halamshauri nyingi zimekuwa zililalamikia kwamba bajeti ni ndogo wakati zimeshindwa kukusanya fedha na kusahau kuwa hicho ni moja ya vyanzo vya mapato ya halmashauri.
aliongeza kuwa TFDA na halmashauri ziendelee kutoaelimu zaidi kwa wananchi ili waweze kutambua kwa urahisi bidhaa zisozofaa na kwa wafanyabiashara ili waweze kutii sheria bila shuruti.
Pamoja na maagizo hayo kwa wakaguzi, katima za chakula na dawa aliwaasa wafanyabiashara kuzingzatia sheria ili kuepuka hasara wanayoweza kupata lakini vilevile wazingatie kuwa wao pia ni sehemu ya jamii.
Awali, mratibu ofisi za kanda na halmashauri TFDA Gloria Omari kuwa mfumo wa kukasimu madaraka kwa halmashauri na mikoa ni moja ya mkakati wa kuongeza wigo wa udhibiti katika nchi zima.
Alisema kuwa kazi ya udhibiti sio rahisi na inahitaji ushirikiano wa karibu kati ya TFDA, mkoa, halmashauri, wananchi kwa ujumla pamoja na waandishi wa habari.
Omari alisema kuwa moja ya malengo ya mafunzo hayo ni kuimarisha utekelezaji wa majukumu na madaraka yaliyokasimiwa kwa halmashauri ili yalete matokeo yaliyokusudiwa.
Aliongeza kuwa lengo nyingine la mafunzo hayo kwa wakaguzi na kamati za chakula na dawa ni kujifunza kanuni mpya na mwongozo wake na mambo mbalimabli yanayohusu udhibiti.
Mamlaka ya chakula na dawa (TFDA)ni wakala wa serikali iliyoanzishwa chini ya kifungu Na. 4(1) cha Sheria Na.1 ya Chakula, Dawa na Vipodozi ya mwaka 2003.
Kwa mujibu wa Sheria hii, TFDA imeanzishwa ili kuimaraisha udhibiti wa usalama, ubora na ufanisi wa chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba
Lengo linguine ni kuhakikisha kwamba bidhaa salama zenye ubora na ufansi unaokubalika ndizo zinazosambazwa na kutumika hapa nchini.