Monday, 3 February 2014

MASHINDANO YA KOMBE LA ANSGARI (ANSGAR CUP) MWAKA 2014 YANUKIA

Dkt Ansgar

Mashindano ya Kombe la Ansgar (Ansgar Cup) tarafa ya Ruvuma, wilayani Songea vijijiin, mkoani Ruvuma yanatarajia kutimua vumbi katika viwanja vya Ansgari vilivyopo Peramiho kuanzia tarehe 13/04/2014 na kumalizika 22/06/2014 Siku ya Ekaristi Takatifu, imefahamika.


Akitangaza ratiba hiyo Kaimu Mwenyekiti wa Mfadhili, Dkt. Magnus Mwanyika wakati kikao cha maandalizi ya mashinadano hayo kulichofanyika jana eneo la Mgahawa wa Peramiho, alisema kuwa mashindano hayo yataanza tarehe 13/04/2014 ngazi ya kata na fainali ngazi ya tarafa yatafanyika siku ya Ekaristi Takatifiu tarehe 22/06/2014.


Dkt. Mwanyika aliwaambia wajumbe kamati ya maandalizi kuwa mwaka kutakuwa na mabadilko kidogo kwa upande wa zawadi , ambapo alifafanua kuwa mshindi wa kwanza atapata zawadi ya 300,000/- (futiboli na netiboli), wa pili ataondoka na shilingi 250,000/- na mshindi wa tatu atajipatia 150,000/- (mpira wa miguu na pete) ukilinganisha na mwaka jana.


“Zawadi mwak huu zimepanda kutoka 250,000. hadi 300,000/- kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili vile vile mwaka huu atapa shilingi laki mbili na nusu toka laki moja na nusu na wa tatu vile vile atajipatia shilingi laki moja na nusu toka shilingi laki moja,” alsiema mwenyekiti huyo.


Alisema kuwa katika ngazi ya kata, zawadi zitakazotolewa ni kwa mshindi wa kwanza na pili tu, ambapo mshindi wa kwanza atapewa shilingi elfu sabini na mshindi wa pili atapaiwa shilingi elfu hamsini kwa mipra wa miguu na pete (Netiboli).


Aliongeza kuwa katika mashindano ya mwaka huu pia kutakuwa na zawadi ya mfungaji bora (best Player) wakati wa fanaili.

“Mfadhili atatoa mipira miwili miwili kwa kila timu itakayoshirika mashindano ya Ansgari mwaka 2014, yaani futuboli na netiboli, mpira moja moja, ngazi ya kata” alifafanua Dkt. Mwanyika.


Kwa upande wa usafiri, Kaimu Mwenyekiti wa Mfadhili alisema kuwa atatoa shilingi laki moja moja kwa timu za Kilagano na Mpnadangindo kutokana na umbali kata hizo ukilinganisha na timu zingine za tarafa ya Ruvuma.


“Kata zingine zitachangiwa shilingi elfu sabini kwa ajili ya kufanyikisha usfari kwa timu zitakazo cheza fainali katoka katani hadi kwenye viwanja vya mashindano,” alisema Dkt. Mwanyika.


Katika hatua nyingine, Kamati ya Maandalizi imemchagua Joseph Mbunda ambaye pia ni Mratibu Elimu Kata ya Maposeni kuwa mwenyekiti mpya baada ya aliyekuwa mwenyekiti Ayubu Mvula kuhamia katika tarafa nyingine nje ya tarafa ya Ruvuma, wakati kwa upande wa katibu, Sixbert Komba ameendelea kushika nafasi ili ile ya ukatibu mpaka mwisho wa mashindano.

Wakati huohuo, Kaimu Afisa wa michezo wa Wilaya ya Songea, Moses Kipanga alizitaka timu zote zitakazoshiriki mashindano mwaka huu kufanya usajili kama sheria ya michezo nchini inavyoelekeza pamoja na kuwa katiba zao.

Alisema kuwa mwaka huu utaratibu umebadilika timu zote zitakazoshiriki mashindano ina lazimika kufanya usajili katika ofisi ua usajili wa vilabu ya wilaya ili kuepuka udanganifu kama wa mwaka jana, ambapo timu nyingi zilikuwa hazina usajili na katiba.

MALENGO YA MASHINDANO

Mashindino hayo hufanikishwa chini ya ufadhali na udhamini wa Mkurugenzi wa Hospitali ya Peramiho Dr. Br. Ansgar Stüfe OSB na kuratibiwa na uongozi wa michezo wa hospitali hiyo. Mashindano huendeshwa kwa kufuata sheria za michezo nchini.

Uendeshaji hufanywa chini ya waheshimiwa madiwani wa tarafa, watendaji wa kata na waratibu wa elimu wa kila kata katika Tarafa ya Ruvuma.

Malengo ya mashindano hayo ni pamoja na kukuza na kuboresha michezo kwa vijana wa kiume na wa kike wa Tarafa ya Ruvuma, kupunguza uzururaji, tabia mbaya hasa za maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, kudumisha undugu na umoja wa kitarafa na kuongeza kipato kupitia biashara ndogondogo wakati wa mashindano.

Mashindano hayo yalishirikisha kata tano za tarafa ya Ruvuma ambazo ni Maposeni, Mpanda-ngindo, Peramiho, Litisha na Kilagano.







WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...