Wakulima wa mahindi kutoka maeneo mbalimabali mkoani Ruvuma wakiwa wamerundika magunia ya mahindi nje ya Maghala ya Taifa mjini Songea barabara ya Songea-Mbinga kusubiri yanunuliwe na serikali. Mkoa wa Ruvuma kati ya mikoa nchini yenye mahindi mengi kutokana na mavuno mazuri lakini yamekosa soko la ndani na kufanya debe moja la mahindi kuuzwa kati ya 2,500/- hadi 3,500/-. Hatimaye serikali imetoa zaidi ya shilingi billioni mbili (2bn/-) kwa ajili ya kununua mahindi ya wakulima mkoani hapa na vilevile serikali imefungua mipaka kwa ajili wakulima waweze kuuza mahindi kwa nchi jirani kwa sharti kutouuza mpaka akiba yao wenyewe.
Marehemu Sista Bernadeta Mbawala OSB wa shirika la masista wabenedikitini wa mtakafu Agnes ya Chipole Wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma, alizaliwa tarehe 27.10.1911 na alikufa tarehe 28.10.1950. maisha ya Bernadeta Mbawala, sista mwafrika, ni wimbo wa kumsifu Baba wa Milele apendaye kuwafumbulia wadogo na wanyonge siri zake.
Sista Maria wa Peramiho (kushoto) pamoja na wakinamama wawili wakiwa kwenye kaburi la Sr. Bernadeta Mbawala aliyezikwa katika Shamba la Mungu karibu na Kanisa Katoliki Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma.
Ingawa habari za maisha yake hazikutangazwa kila siku, watu wengi wanaokana kusali kwenye kaburi lake pamoja na watu wanaosongwa na shida mbalimbali maishani mwao. Hapa Peramiho kuna uvumi wa maneno kwamba, watu wengi wamesaidiwa katika shida zao za kiroho na za mwili kwa maombezi ya Sista Bernadeta. Inaonekana kuwa Sr. Bernadeta napenda hasa kuwasaidia akina mama wasiopata watoto na ambao ndoa zao zipo katika shida.