Tuesday, 28 November 2017

MAKAMU WA RAIS AMTEMBELEA LISSU HOSPITALINI




Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Novemba 28, 2017 amemtembelea mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu aliyelazwa Hospitali ya Nairobi nchini humo.


Msafara wa Samia ulifika hospitalini hapa saa 11.43 jioni akiwa ameambatana na Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk Pindi Chana.


Lissu amelazwa hospitalini hapo akiuguza majeraha ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 aliposhambuliwa Septemba 7 akiwa nyumbani kwake, Area D mjini Dodoma.



Makamu wa Rais amefika hospitalini akiwa njiani kurudi Tanzania baada ya asubuhi kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta. Samia anakuwa kiongozi mkuu wa kwanza wa Serikali ya Tanzania kumtembelea Lissu hospitali tangu alipolazwa usiku wa Septemba 7.

MEYA MANISPAA YA IRINGA KIZIMBANI, WANA CHADEMA WENGINE WATANO WANYIMWA DHAMANA







MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe (Chadema) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Iringa mapema leo akituhumiwa kutishia kumua kwa bastola, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Manispaa ya Iringa, Alphonce Muyinga.


Pamoja na Kimbe, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imewasomea mashtaka matatu wafuasi wengine watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliyofanya Novemba 19 wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kitwiru, Iringa mjini.


Wakati meya huyo ameachiwa kwa dhamana na mahakama ya wilaya Iringa baada ya kusota rumande kwa siku tatu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imewanyima dhamana wafuasi hao watano kwa kuwa kati ya makosa matatu wanayotuhumiwa kuyafanya kosa moja halidhaminiki.


Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Aristeck Mwinyikheri alisema Kimbe aliyefikishwa mahakamani hapo kwa kesi namba 189 ya mwaka 2017 anashitakiwa kutishia kumuua kwa Bastola Katibu huyo wa UVCCM kwa katika tukio lililotokea Novemba 26 mwaka huu katika kata ya Kitwiru, mjini Iringa wakati shughuli ya uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo ikiendelea.


Mwinyikheri alisema meya huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 89 (2) (a) cha kanuni za adhabu.


Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa John Mpitanjia alisema shauri hilo litarudi tena mahakamani hapo Desemba 12, mwaka huu wakati Meya huyo aliyedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akikana kutenda kosa hilo.


Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, wafuasi hao watano wa Chadema walioshitakiwa kupitia kesi namba 190 ya mwaka 2017 na kunyimwa dhamana ni pamoja na Martha Robert, Leonard Kulijira, Esau Bwire, Christopher Jevas na Samwel Nyanda.


Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Richard Kasele , mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo Chakila Felix alisema washitakiwa hao wanatuhumiwa kujeruhi, kuteka na kufanya unyang’anyi kwa kutumia nguvu.


Felix alisema watuhumiwa hao wanatuhumiwa kumjeruhi Dick Frank na kumnyang’anya simu yake ya mkononi.


Mahakama hiyo imewarudisha rumande kwa kuwa kosa la unyang’anyi kwa kutumia nguvu halina dhamana na shauri lao litarudi tena mahakamani hapo Desemba 12, mwaka huu. CREDIT: BONGOLEAKS

THE BREAD OF LIFE SCHOOL PRAISES THE IRINGA DC FOR FOCUSING ON EDUCATION





Bread of Life Secondary School has hailed the leadership of the Iringa District Council by focusing on the education sector in ensuring that the Iringa region enjoys better education and has a nation that has a lot of scholars.

Speaking recently during the school's first school FIRST FORM 4 GRADUATION, school headmaster Pawde Mwasanje on behalf of the board chairman, Bishop of the Evangelical Lutheran Church of Tanzania (KKKT) Iringa Diocese, Blaston Tuluwene Gaville said that without co-operation with Iringa District government, then the school would not have achieved the achievement.

The head of the school said that the school has been very successful since its establishment so he invites other students to join the school.

Mwasanje said that in a Form Two National Assessment (FTNA), the school ranked six among 31 Iringa District schools, in Iringa for a 100 percent pass rate.

He graciously said they registered 19 students to sit for Form Two National Assessment (FTNA); including 11 girls were 8 boys.

For his part, Iringa district Commissioner Richard Kasesela, said that every student should have any skills to succeed in their lives.

The custodian concluded by giving the graduate message through the Bible verse 4:13 "cultivate the education, do not let him go; touch him, for he is your life,’

The School Is situated at KIDETE Village of MGERA ward in Iringa District council, about 10 Kilometers from Iringa Town.



End

TIMU ya soka ya LIPULI FC inakusudia kuwa miongoni mwa timu bora za soka nchini



Akizungumza na wanahabari leo mkoani Iringa Katibu wa LIPULI FC Amon Ellias amesema timu yake kwa sasa ipo katika nafasi nzuri ktk msimamo wa ligi kutokana na juhudi ambazo uongozi ktk timu hiyo umekuwa ukichukua.


"Ukitazama msimamo wa ligi leo utaona nafasi ambayo timu yetu ipo na hiyo yote inakuonyesha juhudi madhubuti tunazochukua kama uongozi kwa pamoja"-Amon alisema.


Alisema moja ya mikakati ambayo inachukuliwa na uongozi ili kuipa timu mafanikio ni pamoja na kutafuta udhamini ili kuondokana na ukata wa fedha.


Amon alisema kwa sasa timu haina mdhamini hali ambayo sio nzuri sana kwa mustakabali wa timu.


"Kama ujuavyo soka la sasa ni lazima lichagizwe na fedha...nasi kwa kuliona hilo tunapambana usiku na mchana kuhakikisha tunapata fedha za kutosha kuhimili mikikimikiki ya ligi kuu"-Alibainisha.


Aidha Amon aliitaja mikakati mingine ambayo ni pamoja na kuhakikisha timu inafanya usajili wa baadhi ya wachezaji ktk kikosi kama sehemu ya kujiimarisha zaidi.


Alisema kupitia dirisha dogo la usajili timu inakusudia kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ili kuwa na safu yenye makali kuliko ilivyo hivi sasa.


"Tumedhamiria kuimarisha safu ya ushambuliaji na tayari benchi la ufundi likiongozwa na kocha msaidizi Suleman Matola tayari wamekwisha tukabidhi sisi kama uongozi mapendekezo yao ya wachezaji wanaohitajika"-Alisema.

SHULE YA BREAD OF LIFE YAIPONGEZA HALMASHAURI YA IRINGA KWA KUJALI ELIMU





Na Friday Simbaya, Iringa

Shule ya Sekondari ya Bread of Life imeupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kuijali vilivyo sekta ya elimu kwa kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Iringa wanapata elimu bora na kuwa na taifa ambalo linakuwa na wasomi wengi.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha nne shule hiyo mkuu wa shule, Pawde Mwasanje kwa niaba ya mwenyekiti wa bodi wa shule, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Mchungaji Blaston Tuluwene Gaville alisema kuwa bila ushirikiano na serikali ya Wilaya ya Iringa, basi shule ya sekondari ya bread of life isingekuwa na mafanikio waliyofikia.

Aidha mkuu wa shule huyo alisema kuwa shule hiyo imekuwa na mafanikio makubwa toka kuanzishwa kwake hivyo anawakaribisha wanafunzi wengine kujiunga na shule hiyo.

Mwasanje alisema kuwa katika mtihani wa kujipima a kidato cha pili, shule hiyo ilishika nafasi ya sita kati ya shule 31 za Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa kwa ufaulu wa asilimia 100.

Mwasanje alisema wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani ya kidato cha pili walikuwa 19 ambapo wasichana 11na wavulana 8.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza tangu kuanzwa kwa shule hayo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa RICHARD KASESELA amesema kuwa kila mwanafunzi anatakiwa kuwa na ujuzi wowote ule ili kufanikiwa katika maisha yao.

Kasesela alimalizia kwa kuwapa wosia wahitimu kupitia mstari wa biblia wa matayo 4:13, ‘Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako,.





WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...