Shule ya Sekondari ya Bread of Life imeupongeza uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa kuijali vilivyo sekta ya elimu kwa kuhakikisha wananchi wa mkoa wa Iringa wanapata elimu bora na kuwa na taifa ambalo linakuwa na wasomi wengi.
Akizungumza hivi karibuni wakati wa mahafali ya kwanza ya Kidato cha nne shule hiyo mkuu wa shule, Pawde Mwasanje kwa niaba ya mwenyekiti wa bodi wa shule, Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Mchungaji Blaston Tuluwene Gaville alisema kuwa bila ushirikiano na serikali ya Wilaya ya Iringa, basi shule ya sekondari ya bread of life isingekuwa na mafanikio waliyofikia.
Aidha mkuu wa shule huyo alisema kuwa shule hiyo imekuwa na mafanikio makubwa toka kuanzishwa kwake hivyo anawakaribisha wanafunzi wengine kujiunga na shule hiyo.
Mwasanje alisema kuwa katika mtihani wa kujipima a kidato cha pili, shule hiyo ilishika nafasi ya sita kati ya shule 31 za Wilaya ya Iringa, mkoani Iringa kwa ufaulu wa asilimia 100.
Mwasanje alisema wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani ya kidato cha pili walikuwa 19 ambapo wasichana 11na wavulana 8.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika mahafali ya kwanza tangu kuanzwa kwa shule hayo ambaye ni mkuu wa wilaya ya Iringa RICHARD KASESELA amesema kuwa kila mwanafunzi anatakiwa kuwa na ujuzi wowote ule ili kufanikiwa katika maisha yao.
Kasesela alimalizia kwa kuwapa wosia wahitimu kupitia mstari wa biblia wa matayo 4:13, ‘Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako,.
No comments:
Post a Comment