Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk Fredrick Shoo amesema Mungu amemjalia Rais Dkt John Pombe Magufuli roho ya kutokuwa na hofu katika utendaji kazi zake.
Askofu Shoo alisema hayo wakati akimwekwa wakfu na kuingizwa kazini Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa jana mjini Iringa.
Alisema kuwa Watanzania walio na nia njema, wanakuelewa na kukubali, na kanisa tunakuombea na tutaendelea kukuombea uzidi kuwa na ujasiri huo, ili Mungu akupe afya njema na usiache kusimama katika lile la kweli kama mwenyewe unavyosema msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Askofu alimalizia kwa kusema, ‘’Tunamuomba Mungu azidi kukupa washauri wema, washauri wasio na unafiki, wasio na hila na malengo ya kujinufaisha binafsi, washauri ambao wanajikomba komba lakini wakiwa na ajenda binafsi.
Ibada ya kuwekwa wakfu kwa Askofu Mteule wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Iringa, Mchungaji Blaston Tuluwene Gavile, ilikufanyika Jumapili Juni 25, 2017 mjini Iringa.
Ibada hiyo, ambayo iliabatana na kuingizwa kazini kwa Msaidizi wa Askofu, Mchungaji Himid Sagga, itafanyika ikiandika historia kwenye Dayosisi hiyo ambapo Askofu Mteule Gavile anachukua nafasi ya Askofu Dkt. Owdenberg Moses Mdegela ambaye amestaafu.
Katibu Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Iringa, Nayman Chavalla, alisema tukio hilo maalum ni la pili katika historia ya Dayosisi hiyo, kwani Mchungaji Gavile anakuwa ndiye askofu wa pili tangu kuanzishwa kwake.
Aidha, katika ibada hiyo Askofu Mteule Blaston Gavile alimuingiza kazini Msaidizi wake Mchungaji Himid John Sagga.
Awali akielezea jinsi ibada hiyo itakavyokuwa, Chavalla alisema itaanza kwa maandamano ya Wachungaji na washarika kutoka Usharika wa Kanisa Kuu Iringa Mjini mpaka viwanja vya Gangilonga ambako ndiko ibada hiyo itafanyika.
"Ibada hiyo inatarajiwa kuongozwa na Mkuu wa KKKT, Askofu Fredrick Shoo akisaidana na Baba Askofu Mstaafu Dkt. Mdegella," alisema.
Pia katika ibada hiyo viongozi wa Makanisa mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi, Wawakilishi wa vyama vya Kimisionari, Viongozi wa Kiserikali, vyama vya siasa, wageni kutoka nchi mbalimbali, wawakilishi wa makampuni na mashirika mbalimbali watahudhuria.
Katibu Mkuu alitoa wito kwa jamii na Wakristo wote kuendelea kuliombea jambo hilo.
Ibada hiyo ilihudhuriwa na wachungaji 210 na wachungaji wastaafu 23 wa kanisa hilo.
Askofu Blaston Tuluwene Gaville alizaliwa tarehe 13.12.1966 katika Kijiji cha Lulanzi, Wilaya ya Kilolo, Mkoa wa Iringa na ni mtoto watatu kuzaliwa katika familia ya Mchungaji Tuluwene Gaville na Asnath Semotto.
Alimuoa Pamella Robert kasencha tarehe 26.10.2002 na familia yake imebarikwa kuwa na watoto wanne , wakiume watatu na mmoja wa kike.