Wednesday, 17 February 2016

WAZIRI WA AFYA MH. UMMY MWALIMU NA NAIBU WAKE WATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI KUKAGUA

Tazama video ya tukio hilo hapa:

muhimbili waziri wa afya
Dk.Stanslaus Ntiyakunze (aliyenyoosha mkono) akiwaonyesha mawaziri namna jengo linavyokarabatiwa ikiwemo miundombinu yake inavyotakiwa kuwa pindi litakapokamilika ikiwemo suala la mfumo wa maji safi na maji taka. Kuliwa kwake ni Naibu Waziri wa Afya Dk Hamisi Kigwangalla wengine Kaimu Mkurugenzi wa hospitali hiyo ya Muhimbili, Prof. Laurance Masaru (kushoto) na Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu (katikati).
Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli wameendelea kufanya kile ambacho wananchi wanataka ikiwemo suala la kutumikia wananchi ambapo mapema leo, Februari 17, Mawaziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu na Naibu wake, Dk. Hamisi Kigwangalla wameweza kutembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kukagua majengo likiwemo lile aliloagiza Rais kuwa litumike kuwa wodi ya akina mama.
Mawaziri hao wamefika Hospitali hiyo ya Taifa majira ya mchana na kisha kupokelewa na wenyeji wao akiwemo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Prof. Laurance Masaru na kisha kukagua moja ya majengo lililopo jengo la watoto ilikuona namna ya kuweza kupunguza msongamano wa wagonjwa katika Hospitali hyo ya Taifa.
Mbali na kukagua majengo pia walipata kuwatembelea wagonjwa na kuwafariji ikiwemo wodi maalum ya wagonjwa wa figo, wodi ya akina mama, wodi ya watoto na upasuaji mdogo pamoja na wodi ya watoto wa ugonjwa wa moyo na ile ya watoto wa ugonjwa wa kansa.
Aidha, Waziri Ummy Mwalimu ameeleza kuwa jengo ambalo Rais ameliagiza litumike kama wodi ya akina mama, amebainisha kuwa agizo hilo wameweza kulitekeleza ndani ya siku moja na awali wamefanikiwa kulaza wagonjwa zaidi ya 40 na hadi kufikia leo wameweza kufikisha wagonjwa 53.
Hata hivyo, Waziri Ummy Mwalimu amewataka wananchi na vyombo vya habari kuwa wavumilivu kwa kipindi cha sasa kwani tayari ukarabati unaendelea kuakikisha miundombinu inawekwa sawa na ndani ya wiki moja itakuwa imekamilika.
Imeandaliwa na Andrew Chale, modewjiblog
muhimbili2
Mkurugenzi wa ufundi, Gaudence Aksante akiwaongoza Mawaziri wa Wizara ya Afya kuelekea katika jengo hilo linalofanyiwa ukarabati ililitumike kwa matumizi zaidi ya wagonjwa kuondoa msongamano hospitali hiyo ya Muhimbili.
muhi
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akipata kuwafariji watoto wanaopatiwa matibabu katika wodi maalum ya matibabu ya kansa.
muimbiliWaziri wa Afya akimjulia hali mmoja wa wagonjwa wanaopatiwa matibabu katika kitengo cha magonjwa maalum ikiwemo Figo. Mgonjwa huyo alipongeza mawaziri hao kwa kuweza kufika hospitalini hapo na kuwajulia hali.
muhimbili33
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati alipotembelea katika wodi ya wagonjwa wa Figo.
muhimbilin77
Waziri Ummy Mwalimu akiwa pamoja na watoto wanaopatiwa matibabu ya ugonjwa wa kansa katika hospitali hiyo ya Muhimbili katika jengo la Watoto.
muhimbili999
Naibu Waziri wa Afya Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Muuguzi mkuu Bi. Praxeda Chenya, wengine ni Waziri Ummy Mwalimu wakati wakiondoka katika jengo hilo la watoto mapema leo Februari 17, 2016.
muhimbili
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof. Laurance Masaru akitoa maelezo namna ya walivyojipanga kuhakikisha wanasaidia wagonjwa wote wanaofika kutibiwa hospitalini hapo. wanaofuata ni Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla na Waziri Ummy Mwalimu pamoja na watendaji wa hospitali hiyo mchana wa leo Februari 17. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog)



Wateja wa Tigo, AzamTV na LigaBBVA kwenda kuangalia mechi ya Barcelona bure



Mtendaji Mkuu wa Azam TV, Rhys Torrington (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Promosheni ya kujishindia safari ya kwenda kushuhudiamechi ya Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga, kati ya Deportivo la Coruna na Barcelona Machi mwaka huu . Katikati yake ni Meneja Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta.Kulia kwake Mkuu wa Idara ya Masoko ya Azam TV, Mgope Kiwanga .Promosheni hiyo ya ushirikiano wa Tigo Pesa na Azam TV, inaanza rasmi leo hadi Machi 13 na washindi wawili watakwenda Hispania.




Tigo, Azam Media na LigaBBVA leo wametangaza ushirikiano baina yao ambao utawapa fursa watumiaji wa huduma Tigo Pesa
wanaonunua vifurushi vya michezo vya AzamTV kupata nafasi ya kusafiri bure bila malipo kwenda kutazama mechi ya ligi kuu kati ya miamba wawili wa Hispania – Barcelon na Deportivo la Coruna
– itakayofanyika Aprili mwaka huu.

Akiongea katika uzinduzi wa promosheni hiyo leo jijini Dar es Salaam, Meneja wa Promosheni wa Tigo Pesa, Mary Rutta amesema, “Kwa kufahamu mapenzi makubwa waliyonayo watanzania kwa mpira wa miguu hasa ligi kuu ya Hispania, Tigo imeungana na Azamtv na LigaBBVA ili kuwapa watanzania, hususan wateja wa Tigo Pesa fursa hii adimu na bure ya kusafiri na kwenda kutazama mechi kati ya Barcelona and Deportivo la Coruna itakayochezwa Aprili 17.”

Rutta alisema: “Mtumiaji wa Tigo Pesa anachohitaji kufanya kushinda fursa hii ni kuhakikisha kimoja kati ya vifurishi vikuu vya AzamTV kipo hewani (Pure, Plus, Play) na hapo atakuwa ameingia katika droo ya kumpata mshindi wa kwenda kushuhudia mechi hii ya kusisimua. Tunapenda kuwahimiza wateja wa Tigo watumiaji wa huduma ya Tigo Pesa kuchangamkia fursa hii ya kusafiri bila malipo kwenda Hispania.”

Tigo, kwa mujibu wa Meneja wa Promosheni wa Tigo Pesa huyo, ina zaidi ya wateja milioni tano waliojisali katika huduma ya Tigo Pesa waliopo kila kona nchini Tanzania

Akiongea katika uzinduzi huo. Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Rhys Torrington alisema, “Kama kawaida yetu, malengo yetu daima ni kuwapa kilicho bora zaidi wateja. Nchini Tanzania tunafahamu ni jinsi gani watu wanavyopumua, kula na kuishi mpira wa miguu na michezo kwa ujumla. 

Hii ni sababu iliyotupa msukumo wa kuleta LigaBBVA ambayo ni mojawapo katika ligi bora duniani kwa mashabiki wengi Tanzania ili kukata kiu yao ya mpira wa miguu.

Alisema “nafasi kama hizi hazijitokezi kila mara kushuhudia maajabu ya Messi, Neymar na Suarez yakitokea”. 

Tunapenda kuwahimiza mashabiki wote wa mpira wa miguu nchini Tanzania kutumia fursa ya kipekee kutimiza kutumiza ndoto zao katika maisha.” Mbali na washinfi wawili watakaosafiri kwenda nchini Hispania katika kipindi cha promosheni hii, aidha zitatolewa zawadi mbalimbali kwa washindi zikiwemo jezi asili za timu ya Barcelona, mipira ya miguu, mipira, tisheti, kalamu, miwani ya jua na zawadi nyinginezo. Ili kushinda zawadi. watazamaji wa mechi za LigaBBVA kupitia AzamTV watahitajika kupiga simu kabla ya mechi kuanza na wakati wa mapumziko na kujibu maswali yatakaokuwa yanaulizwa. 

Torrington alisisitiza “ LigaBBVA ambao tunashirikiana nao, wamefurahishwa na mapokezi mazuri ya watanzania kwa ligi ya ligi ya Uhispania kuanzia siku ya kwanza, na katika kuunga mkono promosheni hii wametukabidhi vifaa vyenye nembo ya LigaBBVA vitakavyotolewa kwa kwa washindi wa kila wiki na tunaamini huu ni mwanzo wa mambo makubwa yajayo.”





TAASISI YA TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) YAZINDUA KAMPENI YA UWIANO WA KIJINSIA



Rais wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) (TWA), Irene Kiwia (katikati ) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) kuhusu uzinduzi wa kampeni ya uwiano wa kijinsia ambayo ni kauli mbiu kuelekea kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, kushoto kwake ni Balozi wa kampeni ya uwiano sawa kijinsia Inspk.Prisca Komba na kulia kwake ni Mwenyekiti wa TWA, Sadaka Gandi kwenye mkutano uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. 



Mwenyekiti wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA), Sadaka Gandi akifafanua jambo kuhusu uzinduzi wa kampeni ya usawa wa kijinsia kwenye mkutano na waaandishi wa habari uliofanyika mapema leo jijini Dar es salaam. 




Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini maelezo kutoka kwa Rais wa TWA Irene Kiwia kuhusu uzinduzi wa kampeni ya usawa wa kijinsia katika mkutano uliofanyika mapema leo Jijini Dar es salaam .





Dar es Salaam, Februari 17, 2016: Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT (TWA) imetangaza uzinduzi wa kampeni ya uwiano wa kijinsia kwenye kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani ya Wanawake inayotoa wito kwa kila mtu kuchukua hatua za dhati kusaidia upatikanaji wa usawa wa jinsia kwa kasi zaidi ili kuwasaidia wanawake na wasichana kufikia malengo yao.


Hali kadhalika inatoa wito kwa jamii kuwa na uongozi ulio na usawa wa kijinsia, kuheshimu na kuthamini tofauti bainia ya jinsia, kuanzisha utamaduni jumuishi na kuondoa upendeleo kwenye sehemu za kazi. 


Akizungumza leo kwenye mkutano wa waandishi wa habari kwenye ofisi za TWA jijini Dar es Salaam Rais wa TWA, Bi. Irene Kiwia alisema kuwa lengo la Kampeni ya Uwiano wa Kijinsia ni kutoa wito kwa wanawake na wanaume kuungana pamoja kusaidia wanawake kufikia hali ya usawa kwa idadi kubwa na kutambua mchango wao usio na ukomo wanaoutoa kwenye uchumi duniani kote kwa ujumla hususani nchini kwetu Tanzania.


“Kampeni ya Uwiano wa Kijinsia inamaanisha kutoa wito kwa wadau wote vikiwemo vyombo vya habari, watu binafsi, serikali na mashirika yote kutambua na kujenga uelewa kuhusu mianya inayozuia mchakato wa kuwepo usawa wa kijinsia na kutaka kuchukua hatua za dhati kuharakisha mabadiliko,” alisema Kiwia.


“Mwaka 2014 Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum -WEF) lilitabiri kuwa usawa wa jinsia duniani utafikiwa mwaka 2095. Lakini mwaka mmoja baadaye, yaani 2015 lilikadiria kuporomoka kwa hatua husika na kupunguza kasi ya kufikia uwiano kuwa pengo la kijinsia linaweza kuzibwa ifikapo mwaka 2133. Hii inamaanisha kusubiri kwa miaka 117 ambayo ni mingi sana. Kutokana na hali hiyo TWA inaungana na wito wa dunia wa kuitaka kila nchi kuliweka suala la jinsia kwenye ajenda zake na kuharakisha kasi ya kufikia lengo la usawa wa kijinsia .” alisema Kiwia.


Akitoa wito kwa watu binafsi, mashirika na wadau wengine kushiriki kwenye kampeni hiyo Mwenyekiti wa TWA Bi. Sadaka Gandi alisema Kampeni itahusisha matembezi ya kilomita sita asubuhi ya siku ya tarehe Tano mwezi March kuanzia kwenye `Viwanja vya Mbio za Mbuzi´ maarufu kama ‘Uwanja wa Farasi’ kupitia kwenye makutano ya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST), kuelekea Kanisa Katoliki la Mt. Petro na kupitia Ubalozi wa Kenya nchini na kurudia sehemu yalipoanzia.


Bi. Sadaka Gandi aliendelea kusema kuwa matembezi hayo yatafuatiwa na mkutano wa kusherehekea siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani ambao utafanyika Machi 6, 2016 kwenye Hoteli ya Regency Kilimanjaro.


Bibi Gandi alisema, “Mkutano huu utawakutanisha wanawake na wanaume kutoka sehemu tofauti ambao watashirikiana na kushawishiana kuungana na harakati hizi, vile vile tutaonyesha mafanikio yaliyopatikana mpaka sasa kutoka Mkutano wa Beijing miaka 21 iliyopita, na hali kadhalika ni kasoro gani ambazo bado zipo na ni kwa namna gani ushirikiano wa pamoja unaweza kuharakisha mabadiliko. Tunaamini mchango wako sio tu kwamba utachangia msingi wa maendeleo ya wanawake bali pia utaonesha ni jinsi gani kampuni yako inachangia kwenye upatikanani wa usawa wa kijinsia kwa ujumla”.


Bibi Gandi alisema kuwa mkutano huo utazungumzia masuala mbalimbali yanayomhusu mwanamke kwa kuzingatia elimu, afya, uongozi, haki na sheria na uchumi.

“Usawa wa jinsia ni muhimu kwa sababu umefungamana na kukua kwa uchumi kwani maendeleo ya wanawake na uongozi ni nguzo ya ufanisi kwenye biashara na ustawi wa uchumi”, alihitimisha. 







DK. KIGWANGALLA AUPA MIEZI SITA UONGOZI WA HOSPITALI YA RUFAA MOROGORO KUREKEBISHA MFUMO WA CHUMBA CHA UPASUAJI


Dk. Kigwangalla akimsikiliza mtoa huduma kwa njia ya mtandao katika malipo (hayupo pichani) alipotembelea hospitalini hapo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro mapema jana Februari 16 na kubaini matatizo mbalimbali ikiwemo chumba cha upasuaji, mfumo wa malipo na ubovu wa vifaa vya maabara.

Dk. Kigwangalla ametoa siku 60 vifaa ndani ya chumba cha upasuaji ziwe zimerekebishwa huku akiagiza ndani ya miezi sita mfumo wa chumba cha upasuaji uwe umetengenezwa vizuri na endapo watashindwa basi atachukua hatua za kufungia vyumba hivyo vya upasuaji kwani vikiendelea kuachwa hivyo vitaendelea kusababisha matatizo Zaidi kwa wanaopaatiwa huduma.

Dk. Kigwangalla akiwa ameambatana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Ritha Lyamuya walitembelea vitengo kadhaa ikiwemo chumba cha upasuaji, jengo la maabara, pamoja na majengo mengine ikiwemo lile la wamama wajawazito na jengo maalum la daraja la kwanza (Grade A).

Hata hivyo ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kushughulikia mara moja mapungufu yaliyobanika. Katika jengo la kuhudumia wagonjwa wa daraja la kwanza, Dk. Kigwangalla alikuta hali ya uchafu na muonekano usiofaa kwa matumizi ya kuitwa daraja la kwanza.

Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, awali lawama nyingi zinatupiwa Wizara yake wakati ukweli ni kuwa Hospitali zipo chi ya Wizara ya TAMISEMI ambao wanashughulikia huku wao Wizara ya afya wakisimamia baadhi ya mambo ikiwemo ukaguzi, madawa, mashine na vifaa.

Dk. Kigwangalla akiangalia namna ya mfumo wa ulipaji kwa kutumia mtandao unavyofanya kazi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro. Wengine ni uongozi wa Hospitali hiyo akiwamo Mganga Mfawidhi, Dk. Ritha Lyamuya.

Dk. Kigwangalla akiangalia mfumo huo wa malipo kwa mtandao hospitalini hapo ambapo hata hivyo ameuagiza uongozi wa Hospitali kuhakikisha wanafunga mifumo ya ulipiaji karibu idara zote za malipo ilikuzuia upotevu wa fedha.

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla akimsisitizia jambo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Ritha Lyamuya kuyafanyia kazi maagizo aliyoyatoa huku akimweleza kuwa atachukua hatua kali endap hayatatekelezwa ikiwemo kufungia huduma za upasuaji. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Morogoro).











REGIONAL WORKSHOP ON MAKING AN IMPACT WITH HUMAN DEVELOPMENT REPORTING STARTS


The host of the workshop, Executive Director of ESRF, Dr. Tausi Kida, presents a paper; The Tanzania human development report experience. The session highlighted the Tanzania report experience in producing the Tanzania human development report 2014/2017.

UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, delivers his speech when opening a four-day regional workshop on making an impact with human development reporting at Ramada Resort in Dar es Salaam, February 16, 2016.

Executive Director of Economic and Social Research Foundation, ESRF, Dr.Tausi Kida congratulates the UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, after he had delivered his opening remarks.

Rodgers Dhliwayo, Economics Adviser/Senior Economist UNDP Tanzania Country Office, presents a paper; Influence of the National Human Development Reports (NHDRs)-Why Produce NHDRs?, during the morning session of four-day regional workshop on making an impact with human development reporting at Ramada Resort in Dar es Salaam, February 16, 2016.

Head of the United Nations Development Programme (Human Development Reports Unit), in New York, Mr. John Hall, presents a paper; The Human Development Approach: An overview of the human development approach, 1990 onwards.





Ice breaker exercise, delegates knowing each other before the start of the crucial session.

Delegate from UNDP-Mozambique, Manuel Filipe, makes his contribution following papers presentation.

A cross section of participants attend the morning session.

UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, (R), exchanges ideas with the, Head of the United Nations Development Programme (Human Development Reports Unit), in New York, Mr. John Hall, during the opening day of four-day regional workshop on making an impact with human development reporting at Ramada Resort in Dar es Salaam Tuesday February 16, 2016.

Mr.Alvaro Rodriguez (seated-R), ESRF Chief, Dr.Tausi Kida, (seated centre), and Rodgers Dhliwayo, in a group photo with some delegates.

UN Resident Coordinator and UNDP Resident Representative in Tanzania, Mr.Alvaro Rodriguez, (L), is being escorted by ESRF Executive Director, Dr. Tausi Kida, as he leaves the workshop venue.




MWENYEKITI WA BODABODA MKOANI MWANZA ATOA TAHADHARI JUU YA VITENDO VYA UKWAPUAJI JIJINI MWANZA



Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda (pichani), amewataharisha
wakazi wa Jiji la Mwanza kuwa makini wawapo barabarani, ili kuepukana na vitendo vya ukwapuaji wa Mikoba na Mabegi vinavyofanywa na baadhi ya wahalifu kwa kutumia pikipiki.

Kayanda alitoa tahadhari hiyo jana Jijini Mwanza baada ya kupokea malalamiko ya kukithiri kwa vitendo vya ukwapuaji vinavyofanywa na baadhi ya watu wanaojifanya waendesha pikipiki, jambo linalochafua taswira ya waendesha pikipiki Mkoani Mwanza.

Tayari watu kadha wamefikisha malalamiko yao kwa uongozi wa bodaboda Mkoani Mwanza, baada ya kukumbwa na kadhia ya kukwapuliwa mikoba pamoja na mabegi yao, ambapo mmoja wa wahanga wa matukio hayo Diana Abdallah ameeleza kukwapuliwa mkoba wake uliokuwa na pesa pamoja na vito vya thamani wakati akitokwa kwenye shughuli zake.

"Nilikuwa maeneo ya Nyegezi ambapo nilikuwa nikitoka kwenye shughuli zangu, nilikwapuliwa mkoba wangu ambao ulikuwa na pesa shilingi Laki Nane, Simu ya shilingi Laki mbili na nusu, Pete sita za Silver zenye thamani ya shili laki moja na elfu ishiri na sita pamoja na miwani ya macho ya shilingi Laki nne. Watuhumiwa waliweza kukamatwa na kesi iko polisi katika kituo cha Igogo".Alisema Abdallah

Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wanaopiga Vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu nchini Edwin Soko, analaani Vitendo hivyo vya ukwapuaji wa Mikoba na Mabegi ya watu kwa kutumia bodaboda ambavyo vimekuwa vikiwakumba watembea kwa miguu Jijini Mwanza, ambapo ameomba jeshi la polisi kutoa ushirikiano wake kwa ajili ya kuvikomesha.

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG.


WANACHACHAMA WA CCM MKOANI MWANZA WAONYA VITEGA UCHUMI VYA CHAMA KUTUMIKA VIBAYA




Wanachama wa Chama cha Mapinduzi CCM, Kata ya Kirumba Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameonya juu ya baadhi ya Wawekezaji nchini wanaotumia Vitega uchumi vya chama hicho bila kufuata mikataba wanayopewa.

Wanachama hao walitoa kauli hiyo wiki hii baada ya Wawekezaji
wanaotumia majengo ya CCM Kata ya Kirumba, kudaiwa kukiuka masharti yao na hivyo kutumia majengo hayo bila kuyalipia kodi ya pango kwa muda mrefu.

Ni kutokana na hatua hiyo, Wanachama hao walichukua maamuzi ya kufunga Majengo hayo ambayo yanatumiwa na Tasisi ya Mikopo ya Wadoki pamoja na Hotel ya Kirumba Resort, huku taratibu nyingine za kisheria zikiendelea, lengo likiwa ni kuhakikisha kwamba watumiaji wa majengo hayo wanayalipia kodivwanayodaiwa vinginevyo watafurushwa nje ya majengo hayo.

Mwenyekiti wa CCM Kata ya Kirumba Abubakary Francis Kweyamba alithibitisha kwamba wanachama hao wamefikia maamuzi hayo, kutokana na kutumia majengo ya chama katika kata hiyo huku wakiwa hawayalipii kodi na hivyo kukisababishia chama usumbufu mkubwa wa kuendesha shughuli zake za kiofisi huku akisisitiza msimamo wa kuendelea kuyafunga majengo hayo.

Katibu Mwenezi wa CCM Kata ya Kirumba Juma Wesa pamoja na Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Ilemela Acheni Maulidi, walisema kuwa maamuzi yaliyochukuliwa na wanachama hayo ni sahihi kwa kuwa malalamiko ya wawekezaji hao yaliishajadiliwa hadi ngazi ya Mkoa ya Chama hicho na kuonekana kwamba wawekezaji hao hawatii makubaliano yaliyofikiwa.

Suala hilo lilifikishwa katika Kituo cha Polisi Kirumba na kila upande umetakiwa kuwasilisha vielelezo vyake ili kutambua wanaokiuka makubaliano ya mkataba wa upangaji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Meneja wa Kirumba Resort hakutaka kuzungumzia malalamiko hayo kwa madai kwamba mzungumzaji ni Mkurugenzi wake ambae alisema amesafiri huku Uongozi wa Wadoki Saccos ukishindwa kupatikana.

PUMBAZUKA NA SIMBAAYA BLOG MAGAZETI YA LEO ALHAMISI


WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...