Dk. Kigwangalla akimsikiliza mtoa huduma kwa njia ya mtandao katika malipo (hayupo pichani) alipotembelea hospitalini hapo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro mapema jana Februari 16 na kubaini matatizo mbalimbali ikiwemo chumba cha upasuaji, mfumo wa malipo na ubovu wa vifaa vya maabara.
Dk. Kigwangalla ametoa siku 60 vifaa ndani ya chumba cha upasuaji ziwe zimerekebishwa huku akiagiza ndani ya miezi sita mfumo wa chumba cha upasuaji uwe umetengenezwa vizuri na endapo watashindwa basi atachukua hatua za kufungia vyumba hivyo vya upasuaji kwani vikiendelea kuachwa hivyo vitaendelea kusababisha matatizo Zaidi kwa wanaopaatiwa huduma.
Dk. Kigwangalla akiwa ameambatana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Ritha Lyamuya walitembelea vitengo kadhaa ikiwemo chumba cha upasuaji, jengo la maabara, pamoja na majengo mengine ikiwemo lile la wamama wajawazito na jengo maalum la daraja la kwanza (Grade A).
Hata hivyo ameutaka uongozi wa Hospitali hiyo kushughulikia mara moja mapungufu yaliyobanika. Katika jengo la kuhudumia wagonjwa wa daraja la kwanza, Dk. Kigwangalla alikuta hali ya uchafu na muonekano usiofaa kwa matumizi ya kuitwa daraja la kwanza.
Dk. Kigwangalla amebainisha kuwa, awali lawama nyingi zinatupiwa Wizara yake wakati ukweli ni kuwa Hospitali zipo chi ya Wizara ya TAMISEMI ambao wanashughulikia huku wao Wizara ya afya wakisimamia baadhi ya mambo ikiwemo ukaguzi, madawa, mashine na vifaa.
Dk. Kigwangalla akiangalia namna ya mfumo wa ulipaji kwa kutumia mtandao unavyofanya kazi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro. Wengine ni uongozi wa Hospitali hiyo akiwamo Mganga Mfawidhi, Dk. Ritha Lyamuya.
Dk. Kigwangalla akiangalia mfumo huo wa malipo kwa mtandao hospitalini hapo ambapo hata hivyo ameuagiza uongozi wa Hospitali kuhakikisha wanafunga mifumo ya ulipiaji karibu idara zote za malipo ilikuzuia upotevu wa fedha.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Kigwangalla akimsisitizia jambo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Dk. Ritha Lyamuya kuyafanyia kazi maagizo aliyoyatoa huku akimweleza kuwa atachukua hatua kali endap hayatatekelezwa ikiwemo kufungia huduma za upasuaji. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Morogoro).
No comments:
Post a Comment