Wednesday, 30 September 2015

MSAFARA WA LOWASSA WASIMAMISHWA ZAIDI YA MARA NNE AKITOKEA TANGA KUELEKA DAR

Msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ukichanja mbuga kutokea jijini Tanga kuelekea jijini Dar es salaam mapema asubuhi juzi.

Sehemu ya wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, wakiwa wamefunga barabara, wakimtaka Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea jijini Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, waliofunga barabara ili azungumze nao leo Septemba 29, 2015, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.PICHA NA OTHMAN MICHUZI.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muheza wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).



Umati wa wakazi wa mji wa Muheza.
Ilikuwa ni furaha kwa kila aliemuona Mh. Lowassa alipokuwa akizungumza nao.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Mji wa Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kuzungumza nao, wakati akiwa safarini kwa kuelekea Dar es salaam kwa njia ya barabara akitokea Mkoani Tanga.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake leo Septemba 29, 2015.
Waziri Mkuu wa zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Mji wa Korogwe, Mkoani Tanga, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Walimu Korogwe, Mkoani Tanga leo Septemba 29, 2015.




MAGUFULI ATINGISHA DODOMA MJINI MKUTANO WAKE WAFURIKA KULIKO KAWAIDA



Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa jamhuri tayari kuhutubia wakazi wa Dodoma mjini.


Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Dodoma mjini waliofurika kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika ndani ya uwanja wa Jamhuri mjini hapo.


Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akielezea umuhimu wa amani katika Taifa letu na kusema kuna umuhimu wananchi kujifunza historia kabla ya kuwania nafasi mbali mbali za uongozi kwani itasaidia kutunza na kuilinda misingi iliyowekwa na waasisi wa Taifa hili.

Warioba alimpongeza sana mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwa kuhubiri amani katika kila mkutano wake wa kampeni kitu ambacho kinasaidia sana kuwakumbusha wananchi wa Tanzania kudumisha na kuitunza amani kati yetu.


Mgombea Ubunge jimbo la Dodoma mjini akimuelezea Mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli changamoto mbali mbali za Dodoma mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapo.


Mgombea ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Ndugu Anthony Mavunde akihutubia wakazi wa Dodoma mjini mbele ya mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapo.


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Abdalla Bulembo akihutubia wakazi wa Dodoma mjini kwenye mkutano wa kampeni za kumnadi mgombea urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Jamhuri mjini hapo.


Mgombea wa Ubunge jimbo la Dodoma mjini Anthony Mavunde akicheza muziki wa vijana wa Temeke mtindo maarufu unaojulikana kama mapanga shaa sambamba na Chegge na Temba .


Mtayarishaji wa Muziki wa Kizazi kipya P Funky Majani akiwasalimu wakazi wa Dodoma na kuwaambia kila mmoja wao ana jukumu la kumpigia kura mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli.


Ali Kiba katikati akiimba na kucheza pamoja na wacheza show wake kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofnyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.


Msanii Tunda Man akitumbuiza kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.


Wahamasishaji wakicheza wakati wa mkutano wa kampeni za CCM.


Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli (wa pili kushoto)akiwa jukwaani pamoja na viongozi wengine ,Mawaziri Wakuu wastaafu Jaji Joseph Warioba, Mzee Samuel Malecela, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Adam Kimbisa na Mgombea Ubunge wa jimbo la Dodoma mjini Ndugu Anthony Mavunde.


Mgombea Ubunge wa jimbo la Mtera Ndugu Livingstone Lusinde akipiga push up kama ishara ya kumuunga mkono mgombea urais kwa tiketi ya CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.

UBA’S ODUOZA WINS CEO OF THE YEAR AWARD AT INVESTMENT SUMMIT IN NEW YORK



Group Managing Director and CEO, UBA Plc, Mr. Phillips Oduoza.

Group Managing Director and CEO, UBA Plc, Mr. Phillips Oduoza has emerged the 2015 Ai Socially Responsible Investment (SRI) 30 CEO of the year at this year's 8th annual Ai CEO Investment Summit. This is the second time he is winning the award after winning it first in 2013.

He was named the winner from a long shortlist that included Nassef Sawiris, CEO, Orascom Construction Company, Sifiso Dabengwa, CEO, MTN Group, SA, Guillaume Roux, CEO, Lafarge Africa, Segun Agbaje, CEO, GT Bank, Graham Clark, GMD, Dangote Sugar and Ben Kruger/Sim Tshabalala, Co-CEOs, Standard Bank. The event took place in New York at the sidelines of the UN General Assembly.

Africa investor (Ai), is a leading international investment and communications group based in South Africa. Every year it organises the institutional investment summit as a platform for public and private sector leaders in Africa to dialogue with global counterparts on ways to invest and grow businesses in Africa. As an integral part of the summit, Ai also hosts the investment and business leadership awards to reward exceptional business practices, economic achievements and investments across Africa, whilst recognising the institutions and individuals improving the continent’s investment climate.

At the summit and awards ceremony attended by over 250 of Africa’s most prominent and influential business, government and development finance leaders, as well as five African Heads of State, the UBA CEO won the Ai SRI CEO of the Year award in recognition of his exceptional achievements over the last year which according to the summit organisers, is an “inspiration for business and government leaders working to raise Africa’s investment profile”.

The judging panel considered excellent leadership skills, enhanced organisational image, innovation and originality as well as alignment with the millennium development goals (MDGs) in choosing the Socially Responsible Investment (SRI) 30 CEO of the year. Speaking on the award, Oduoza who has twice been recipient(the first time in 2013), said: 'as Africa’s global bank, The United Bank for Africa, UBA, has operations in 19 African countries and 3 global financial centres - New York, London and Paris, serving over 9 million customers. This award validates our efforts over the years in building a solid pan-African banking business that is profitable, sustainable and socially responsible. I dedicate it to all UBA people: customers, staff and other stakeholders in Africa and across the globe". 

Other recognitions at the ceremony include: Venture Capital/Private Equity Award won by the Abraaj Group, whilst Institutional Investor of the Year and Investment Promotion Agency of the Year went to Public Investment Corporation of South Africa (PIC) and Centre de Promotion des Investissementsen Côte d'Ivoire (CEPICI) respectively. The Leadership in Sustainable Investment in Africa Award went to the Bill and Melinda Gates Foundation.


Uganda President Yoweri Museveni with General Manager USA.

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...