Na Friday Simbaya,
Songea
MKOA wa Ruvuma hivi karibuni walikuwa na Mkutano Mkuu wa Wadau wa Kutathmini maendeleo ya elimu mkoani mwaka 2011, uliyofanyika hapa Peramiho katika Halmashauri ya Songea.
Mkutano huu ulilenga kutathmini utekelezaji wa kazi na kupima ufanisi wa shughuli za maendeleo ya elimu mkoani hapa.
Aidhi, kuanzia mwaka 2008 kumekuwepo pia mikutano ya wadau ya kutathmini maendeleo ya elimu ngazi ya wilaya/ halmashauri, kata na shule; ambao hufanyika kabla ya kikao cha tathmini ya kimkoa.
Akifungua mkutano huo mkuu wa wadu wa elimu wa kutathmini maendeleo ya elimu, mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dkt. Christine Ishengoma aliwaambia wadau kwamba jambo la msingi ni kueleza ukweli, ili kupata hali halisi ya utekelezaji wa vitendo uliyofanyika, na sio taarifa za maandishi au maneno tu, tofauti na uhalisia.
Alisema kuwa lengo hasa la kufanya tathmini katika ngazi zote hizo ni kupima utekelezaji wa mipango na malengo waliyojiwekea kwa kipindi kilichopita; kwa kuzingitia eneo husika katika MKUKUTA, Dira ya Maendeleo ya taifa ya 2025 na Malengo ya Maendeleo ya Milenia.
“Malengo hayo ni pamoja na kupima ubora wa kazi, kubaini mafanyikio na changamoto na kujiwekea mikakati ya utekelezaji kwa kipindi kinachofuata,” alielezia mkuu wa huyo wa mkoa.
Mikutano hii imekuwa ikifanyika katika halmashauri tofauti, kwa kuhusisha ziara katika asasi za kielimu. Lengo hasa ni kujua hali halisi ya mazingira ya kutolea elimu kwa kubaini mafanyikio na changamoto zinazojitokeza katika mazingira hayo.
Aidha, mkutano wa mwaka 2011, tofauti na maka jana, unalenga katika mazingira ambayo mkoa umefanyavibaya katika matokeo ya mitihani ya elimu ya msingi na sekondari mwaka 2010. Katika Mitihani wa Elimu ya Msingi (Darasa la VII) wastani wa ufaulu kimkoa ulikuwa asilimia 48 tu, ikiliganishwa na wastani wa ufaulu kitaifa wa asilimia 53.5.
Mitihani wa sekondari Kidatocha nne, wastani wa ufaulu kimkoa ni asilimia 45.32 ikilinganishwa na wastani wa kitaifa wa asilimia 50.4.
Kufuatia hatua hiyo, Mkoa wa Mkoa wa Ruvuma Dkt. Ishengoma waliwaomba wanaohusiki na utekelezaji wawekke dhamira ya kweli ya kutekeleza kwa vitendo wa kufanya ufuatiliaji wa karibu na kuchukuwa hatua stahili.
Pamoja na masuala ya elimu, mkuu huyo wa mkoa walizungumzia pia umhuhimi wa mazingira kwa uhai wa taifa. Aliwakumbusha wadau wa kikao kwa kutunza mazingira kuwa masafi, kutunza vyanzo vya maji, misitu ya asili na kupanda mingine pale inapokosekana.
“Tunze mazingira ya shule zetu pia kwa kupanda miti, maua na ukoka ili kuboresha mandhari ya shule, kila shule iwe na bendi, viwanja na vifaa vya michezo, kuwepo pia na programu ya chakula; ili kuvutia wanafunzi kuhudhuria shule ni pamoja na kujenga afya zao” alisema.
Kwa upande wa UKIMWI, alisema ukimwi bado ni tatizo kubwa kwa Tanzania, hasa mkoa wa Ruvuma na Halmashauri zote. Mkoa wa Ruvuma bado una kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU kwa kuwa na asilimia 6.3, ambapo kitaifa ni asilimia 5.7.
Alisema, bado taifa linaendelea kupoteza nguvu kazi ya wataalam wa sekta zote, wakiwemo wataalam wa sekta ya elimu. Aidhi, Ukimwi unamaliza jamii ya watanzania kwa ujumla wakiwemo wazazi na kuacha yatima, ambao pamoja na matatizo mengine yanayowakumba, wanaathirika pia kielimu.
Kwa kuzingatia hayo, waliwasihi wote kuwa makini kuepuka janga hili, ikwa pamoja na kupima afya kwa wale amabo bado, au waliopima muda mrefu uliyopita.
Wakati huohuo, afisa Elimu wa Wilaya Songea, mkoani Ruvuma Bw. Richard Mtoni amepiga marufuku walimu kutoka nje ya kituo cha kazi bila vibali kutoka kwa wakuu wa shule za msingi zao.
Afisa huyo wa elimu alitoa rai jana wakati wa mkutano wa kielimu wa kuthamini maendeleo ya elimu katika wilaya ya songea pamoja na kutathamini matokeo ya darasa la saba ya mwaka jana (2010) ngazi ya kata, uliyoshirikisha wadau mbalimbali wa elimu kutoka kata za Maposeni na Peramiho.
Hatua huyo ya kutaka wakuu wa shule za msingi kutoa vibali kwa walimu pindi wapoomba ruhusa kwenda mahali kutokana wilaya huyo kfanya vibaya katika mtihani wa darasa la saba mwaka jana, kwa lengo la kuinua kiwango cha ufaulu kwa watoto.
Wilaya ya Songea katika ya wilaya zilizofanya vibaya katika mtihani wa darasa la saba kimkoa kwa kushika nafasi ya ya tano katika wilaya tano za Songea Mjini, Namtumbo, Mbinga, Tunduru pamoja na yenyewe Songea Vijijini.
“Kuna utaratibu uliyzuka kwa walimu kutumia muda mwingi kufanya biashara zao binafsi kuliko kufanya kazi ya walimu wakati muda wa kazi. Utakuta mwalimu naondika kituoni kihoelela bila kumshirikisha mwalimu mkuu wake kwenda mjini kufanya kazi binfsi na kuwaacha wanafunzi bila kusoma, naweza kuta shule moja walimu watano wote hapa wametoka na waacha wanafunzi peke yao……” alisema Bw. Mtoni.
Aidha, alisema kuwa pamoja na mambo yanayoshusha kiwango cha taaluma na kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi wa wilaya ni pamoja walimu kutojitoa kufundisha kwa moyo na kufanyakazi kwa mazoea.
Akisoma taarifa ya maendeleo ya elimu ya wilaya ya songea, afisa elimu wa wilaya (Taaluma), Bw. Vincent kayombo, alisema kuwa wilaya songea imeshika nafasi ya mwisho kimkoa katika mtihani wa darasa la saba 2010, kwa ufaulu ukilinganisha na wilaya zingine za Mkoa wa Ruvuma.
Bw. Kayombo alisema, wilaya ya songea kiwango cha ufaulu cha wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi kimeshuka kutoka asilimia 69 mwaka 2009 hadi kufikia asilimia 39.4 mwaka 2010, sawa sawa na asilimia 59 wahitimu waliyofeli.
Alisema kuwa kata za Maposeni na Peramiho ni mmoja za kata 16 za wilaya songea ambazo hazikufaulisha wanafunzi wa darasa la saba mwaka jana kwa kiwango cha kuridhisha ukilinganisha na Kata ya Mahenje inayoongoza kwa fanya vizuri wilayani hapa kwa miaka mitatu sasa.
Katika masomo amabayo wanafunzi wanafanya vibaya katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi pamoja na mosomo ya Hesabati, Sayansi, Maarifa ya Jamii na Kiingereza.
“Sisi ka walimu tunapaswa wa kuweka bidii katika kazi wetu, tunatakiwa kuipenda kazi kwa hiyo wanafunzi kwa viwango vinavyotakiwa ili tuweze kuwa kupandisha kiwango cha ufaulu pamoja na kuborasha ubora wa taaluma kwa wanafunzi, hatimaye kuleta kupandisha hadith way wailaya yetu” alisema Bw. Kayombo.
Subscribe to:
Posts (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...