Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza katika maadhimisho ya Uhuru wa habari duniani yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Umoja wa Vilabu vya waandishi wa Habari nchini (UTPC), Jane Mihanji, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Bw. Ernest Sungura, Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalon Kibanda akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Maelezo, Assah Mwambene akizungumza katika maadhimisho hayo.
Kaimu Meneja wa Uhuru FM, Angela Akilimali (kulia) pamoja na wadau wa vyombo vya habari katika maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani.
Kutoka kushoto ni Mshauri wa Masuala ya Habari Umoja wa Ulaya, Susane Mbise na Mshauri wa Masuala ya Mawasiliano Umoja wa Mataifa (UN), Hoyce Temu wakifuatilia mijadala katika mkutano huo.
Mwanahabari na Bloga, Maggid Mjengwa akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Mello akizungumza.
Meza kuu katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Habari Duniani.
Na Joachim Mushi, Morogoro
UMOJA wa Nchi za Ulaya nchini Tanzania (EU) umepinga vikali vitendo vya kikatili na unyanyasaji ambavyo wamekuwa wakifanyiwa waandishi wa habari na vyombo vya dola vya Serikali wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao ambapo ilitokea mwanahabari mmoja kuuwawa. Alisema hawatachoka kukemea matukio hayo ya unyanyasaji kwani yanafifisha uhuru wa habari.