Tuesday, 7 June 2016

HIFADHI YA TAIFA YA RUAHA KINARA KWA UJANGILI WA TEMBO NCHINI

Mwalimu wa Uchumi na Utalii Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM),  Profesa Wineaster Anderson (kulia), akitoa mada kuhusu uchumi na Utalii katika mkutano wa mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na wanahabari waandamizi kutoka vyombo mbalimbali mjini Morogoro leo.
Mkurugenzi wa Utalii na Masoko wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Ibrahim Mussa (kulia), akitoa mada katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Dk. Felician Kilahama (kulia), akitoa mada kuhusu misitu katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Dk.Allan Kijazi, akizungumza jana katika mkutano huo.
Wanahabari Khadija Khalili (kushoto) na Beatrice wakiwa kwenye mkutano huo.
Wahariri, Bakari Kimwaga (kushoto) na Anicetus Mwesa wakifuatilia mkutano huo.


Mwanahabari Lazaro kulia akijiandikisha katika kitabu cha mahudhurio
Wanahabari na wahariri wakiwa kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha wamiliki wa Blogu Tanzania (TBN), Joachim Mushi akiwa kazini katika mkutano huo ulihudhuriwa na baadhi ya bloger.
Mhariri wa Nipashe, Jesey Kwayu akiuliza maswali.
Mwanahabari na mpiga picha wa gazeti la mtanzania, Humphrey Shao akiuliza maswali.
'Hapa ni kazi tu' wanahabari wakichukua taarifa mbalimbali za mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

MKURUGENZI Mkuu wa Hifadhi za Taifa (Tanapa), Dk. Allain Kijazi amesema Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ni kinara wa ujangili wa Tembo ukilinganisha na hifanyi nyingine

Dk. Kijazi ameyasema hayo leo mkoani Morogoro katika siku ya pili ya Mkutano wa Mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania ulioandaliwa kwa kwa ajili ya wahariri na wanahabari waandamizi wa vyombo mbalimbali vya habari.

"Hali hii ya  ujangili inatokana na kuwepo kwa tembo wengi ambapo majangili wamekuwa wakiingia katika hifadhi hiyo na kufanya uharifu" alisema Kijazi.

Aliongeza kuwa kutokana na hali hiyo jitihada kubwa zinafanya kwa kutumia mfumo wa kiokorojia kwa lengo la kuhakikisha udhibiti wa ujangili unafanikiwa na kunusuru ujangili huo unaotishia katika hifanyi hiyo.


Katika hatua nyingine Dk.Kijazi ametoa mwito kwa Serikali kutengeneza miundo mbinu ya barabara na Wawekezaji kujenga mahoteli katika mikoa ya Kusini na Magharibi mwa Tanzania ili kukuza utalii katika maeneo hayo jambo litakalo inua uchumi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa baadhi ya mikoa ya Kusini na Magharibi mbayo inavivutio vya utalii lakini imeshindwa kufanya vizuri katika kuingiza watalii wengi kutokana na miondo mbinu yake ya barabara kutokuwa rafiki.

"Ninaamini waandishi wa habari mkitupigia debe na Serikali ikasikilia kilio hiki na kutengeneza barabara kwa kiwango kizuri na Wawekezaji wakajenga mahoteli hakika itasaidia kuvutia watalii kama ilivyo kwa mikoa ya Kaskazini," alisema.

Alifafanua kuwa mikoa ya Kaskazini ambayo inavivutio imekuwa ikipata watalii wengi kutokana na urahisi wake kufikika kwa maana watalii wanahitaji kutumia muda mfupi kufika mbugani ili atumie muda mrefu kuona wanyama.

Aliongeza kuwa hali hiyo ni tofauti na mikoa ya Kusini na Magharibi ambako mtalii atatumia murefu barabarani na kutumia muda mfupi katika kuangalia wanyama na vivutio vingine jambo ambalo si lengo lake.

Alisema licha miundo mbinu ya barabara za Kusini kutokuwa rafiki kufika katika vivutio, pia hata malazi kwa watalii si ya kuvutia na pengine hakuna kabisa hivyo ni changamoto kwa wawekezaji kuhakikisha wanajenga mahoteli ya kisasa.

Aliweka wazi kuwa ikiwa jambo hilo litafanikiwa kwa kuwa na miundombinu mizuri ya barabara na hoteli zenye viwango hakika watalii katika mikoa ya Kusini wataongezeka.


Wakati huo huo, Mkurugenzi wa Masoko Tanapa, Ibrahimu Mussa alisema kuwa ili kuinua mapato yanayotokana na utalii nchini malipo ya watalii yanafanyika kwa kadi za kibenki.

"Tumeamua kuondokana na upokeaji wa fedha kwa 'Cash' ili kuondoa upotevu wa mapato jambo litakalosaidia kuinua kiwango cha ukusanyaji wa mapato tofauti na ilivyokuwa awali,"alisema.

Akizungumzia suala baadhi ya watalii kulipia gharama viingilio wakiwa nchini kwao, alisema fedha wanazolipa zinafika Tanzania na lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha watalii wanakuwa salama katika mali zao.

Aliongeza kuwa hata mtalii akiumia akiwa hapa nchini akiwa kwenye utalii analipwa bima kupitia nchi yake jambo ambalo linamfanya kuwa salama zaidi.

Pia alisema Tanzania imeshuka katika viwango vya vivutio vya asili ikitoka namba mbili nyuma ya Brazil hadi na namba saba na katika viwango vya jumla inashika nafasi ya 93 kati ya nchi 114 zenye ushindani.

Alifafanua kuwa sababu ya kushuka katika viwango hivyo vya dunia ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo uvamizi wa maeneo ya vivutio hivyo na miundo mbinu ya barabara na changamoto zingine zilizopo.



WAFUGAJI WADOGO WALIA NA BEI NDOGO YA MAZIWA




Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Ushirika (WKMU) sehemu ya mifugo, Dkt. Maria Mashingo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa mfugaji wa mdogo wa ng'ombe wa maziwa mjini Njombe Paul Kasunga alipotembelea banda hilo maonesho wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unywaji wa maziwa yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe wiki iliyopita. (Picha na Friday Simbaya) 




Ng'ombe wa maziwa aina ya Ayshire ambaye ana umri miaka mitano anauwezo wakutoa lita 22 ya maziwa kwa siku. 






Small milk producer Wema Gilbert Ngimbuchi (blind) of Ikuna Village Ikuna in Ward, Njombe district sings before the Permanent Secretary in the Ministry of Agriculture, livestock and Cooperatives (livestock section) Dr. Mary Mashingo (left) as a sign of thankfulness after she was handed over a registration certificate as a milk producer supplied by Tanzania Dairy Board (TDB) during the peak week of drinking milk made nationally in Njombe region last week. The Staff of the East Africa Dairy Development (EADD II) for their unity, they performed an act of mercy by the presenting a cow to her (Wema Ngimbuchi) worth Tsh. 1,000,000/=. (Photo by Friday Simbaya)





Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Ushirika (sehemu ya mifugo) Dkt. Maria Mashingo (kushoto) akipeana mkono na mzalishaji mdogo wa ng'ombe wa maziwa Wema Gilbert Ngimbuchi (mlemavu wa macho) wa Kijiji cha Ikuna Kata ya Ikuna, wilyani Njombe, mkoani Njommbe baada ya kumkabidhi cheti cha usajili cha mzalishaji mdogo wa maziwa kilichotolewa na Bodi ya Maziwa Tanzania (TDB) wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya unywaji wa maziwa yaliyofanyika kitaifa mkoani Njombe wiki iliyopita. Wafanyakazi wa Mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa Afrika Mashariki (EADD II) awamu ya pili kwa umoja wao,walifanya tendo la huruma kwa kumzawadia mfuaji huyo mtamba wa ng`ombe mwenye thamani ya Tsh. 1,000,000/=. (Picha na Friday Simbaya)






Permanent Secretary in the Ministry of Agriculture, livestock and Cooperatives (livestock section) Dr. Mary Mashingo (left) shakes hand with small milk producer Wema Gilbert Ngimbuchi (blind) of Ikuna Village Ikuna in Ward, Njombe district, after handed over a registration certificate as a milk producer supplied by Tanzania Dairy Board (TDB) during the peak week of drinking milk made nationally in Njombe region last week. The Staff of the East Africa Dairy Development (EADD II) for their unity, they performed an act of mercy by the presenting a cow to her (Wema Ngimbuchi)worth Tsh. 1,000,000/=. (Photo by Friday Simbaya) 




Baadhi ya wafanyakazi wa Mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa Afrika Mashariki (EADD II) kutoka mikoa ya Mbeya, Njombe na Iringa wakiwa katika picha ya pamoja.




Mfugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka kitovu (dairy hub) kutoka kikundi cha wafugaji wadogo Halmashauri ya Njombe (WAWAHANJO) katika kijiji cha Ikando Rahel Mhema akiongea na mwandishi wa habari nyumbani kwake katika Ikando wilaya Njombe mkoani njombe.










Mfugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka kitovu (dairy hub) kutoka kikundi cha wafugaji wadogo Halmashauri ya Njombe (WAWAHANJO) katika kijiji cha Ikando Rahel Mhema akionesha marobota yako ya hei (majani ya Rhodes boma) katika sehemu kavu iliyoezekwa kuzuia jua na mvua alipotembelewa na mwandishi wa habari hivi karibuni. Mfugaji huyo alipata mafunzo ya dhana ya kutengeneza hei kwa njia rahisi ya kufunga marobota ya hei kwa njia mkono kutoka Mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa Afrika Mashariki (EADD II) awamu wa pili kwa kushirikana na Heifer International.

























Mfugaji wa ng’ombe wa maziwa kutoka kikundi cha wafugaji wadogo cha mshikamano Efrahana Kidenya katika kijiji cha Mhaji wilayani Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe akiwa katika shamba la ekari moja la malisho la majani (hei) aina ya Rhodes boma. 




Ndama aliyezaliwa kwa njia Uhimilishaji












Bustani ya mboga za majani (kitchen garden).






Mshauri mwandamizi wa biashara kutoka EADD II mkoa wa Njombe Joseph Lyamuya (kulia) akiwa mfugaji kutoka katika kijiji cha Mlevela kata ya Igima wilayani Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe.












Mfugaji wa ng’ombe wa maziwa Catherine Mlowe akiwa na mme wake kutoka katika kijiji cha Mlevela kata ya Igima wilayani Wanging’ombe, Mkoa wa Njombe akionesha sehemu ya kuhifadhia mkojo wa ng’ombe kutoka banda la ng'ombe unayotumika kama mbolea kwenye bustani ya mboga za majani (kitchen garden).




Mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa afrika mashariki (EADD II) awamu ya pili umeinua kipato cha wafugaji wa ng’ombe wa maziwa katika mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya kwa kuwajengea uwezo wa kutumia fursa ya kukusanya maziwa kwa pamoja, kupata mafunzo na huduma mbalimbali za ufugaji na biashara ya maziwa kupitia vyama vya wafugaji.

Meneja wa mradi nchini Mark Tsoxo aliwaambia mtandao wa SIMBAYABLOG jana kuwa mradi huo umeweza kufanya wafugaji wadogo wa ng’ombe wa maziwa kuwa na mahali pakukusanyia na kuhifadhi maziwa kwa wingi (dairy hubs), upatikanaji wa huduma za kinga na tiba ya mifugo, uboreshaji wa koosafu (breeding line) ya ng’ombe, upatikanaji wa mbegu za malisho, vyakula vya ziada vya mifugo pamoja na kutoa ushauri na huduma za ugani.


Tsoxo alisema kuwa EADD II itawawezesha wafugaji kitaalamu kutumia teknolojia mpya na stadi za uzalishaji malisho, kuwa na vyanzo mbadala vya vyakula bora vya mifugo, ukusanyaji, upoozaji na usafirishaji wa maziwa.


Alisema kuwa mradi huu wa EADD II utaweka kupaumbele katika kuuganisha nguvu ya pamoja ya wafugaji na usawa wa kijinsia ili kuongeza tija kuwanufaisha walengwa katika kaya zipato 136,000 katika Afrika Mashairiki na jamii kwa ujumla. Kwa Tanzania mradi umelenga kunufaisha kaya 35,000. 


Mradi huu unatekelezwa na ushirikiano baina ya mashirika matano ya maendeleo. Mashirika hayo ni Heifer International Tanzania (ushauri na huduma za ugani), Technoserve (ushauri wa biashara na masoko), ICRAF (mazingira na malisho), African Breeders Service (Uhimilishaji) na International Livestock Research Institute (Masuala ya utafiti) 

http://www.heifer.org/campaign/fund-a-project/east-africa-dairy-development-ii.html





UN yawapiga msasa wanafunzi wa UDOM kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)





Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akiendesha semina fupi kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) (hawapo pichani) inayoendelea mjini Dodoma chuoni hapa.






Katika kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo yanatakiwa kumfikia mtu mmoja mmoja, ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini (UN) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), mafunzo ambayo yataweza kuwajengea uwezo kuhusu mpango huo na jinsi unavyoweza kubadili maisha yao.






Akizungumza na MO blog kuhusu mafunzo hayo, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, Bi. Hoyce Temu alisema kuwa mafunzo hayo kwa wanafunzi wa UDOM ni sehemu wa mafunzo ambayo yanatolewa na ofisi ya UN nchini ili kuwawezesha Watanzania kuufahamu mpango huo ambao una malengo ya kubadili maisha ya kila mwananchi, mpango ambao utamalizika mwaka 2030.






Alisema katika mafunzo hayo wametoa elimu kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) kwa wanafunzi zaidi ya 200 na hayo siyo mafunzo ya kwanza kwani wameshatoa mafunzo kama hayo kwa wabunge wa Tanzania lakini pia wameshafanya mafunzo kama hayo jijini Arusha ambapo yalihudhuriwa na vijana zaidi ya 200.






“Tunataka kila Mtanzania ajue kuhusu Malengo ya Maendeleo Eendelevu (SDGs) tumeshatoa elimu sehemu nyingine hii siyo ya kwanza na tutaendelea kwenda maeneo mengine kutoa elimu zaidi na katika hilo ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini ipo imejipanga kufanya hivyo,” alisema Bi. Temu.


Nae Mkuu wa Kitovu cha Mitaala katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Willy Komba alisema mafunzo hayo yamewajenga na kupata elimu ambayo walikuwa hawajaipata awali inayohusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na pia kueleza kutokana na umuhimu wake watakaa kuangalia ni jinsi gani wataweka katika mtaala wa masomo ili wanafunzi wajifunze kuhusu SDGs.






“Sababu na mimi ndiyo Mkuu wa kitengo cha mitaala nitakaa na wenzangu tuone jinsi gani tunaweza kuweka katika mitaala yetu ili hata wanafunzi wajifunze kama masomo, tunawashukuru kwa mafunzo yenu mmetupa changamoto mpya ambayo hatukuwa nayo,” alisema Komba.








Sehemu ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakisiliza kwa makini wakati semina fupi kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) iliyoendeshwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).




Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa wakufunzi wa masuala ya SDGs, Hoyce Temu akifafanua jambo wakati wa semina fupi ilihusisha wanafunzi wa UDOM inayoendelea mjini Dodoma.




Mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDOM wa Didgrii ya kwanza ya Mifumo ya habari na Mawasiliano, Lobezi Kulilo akihoji kuhusiana elimu ya SDGs kuwafikia watu walio vijijini.




Mwanafunzi wa Digrii ya kwanza ya Sayansi ya Kompyuta UDOM, Traygod Lyimo akiuliza swali kwa wakufunzi kuhusiana na SDGs.




Pichani juu na chini ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakipitia vipeperushi mbalimbali vyenye taarifa za kina kuhusu Malengo 17 mapya ya Maendeleo Endelevu (SDGs) wakati wa semina fupi iliyoandaliwa na Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini.














Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, akijibu baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wanafunzi wa UDOM wakati wa semina fupi kuhusu Malengo ya dunia iliyoandaliwa na Umoja huo mjini Dodoma jana.




Mkuu wa Kitovu cha Mitaala katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Prof. Willy Komba akitoa neno la shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuwapatia mafunzo ya SDGs mara baada ya kumalizika semina fupi kwa wanafunzi wa UDOM.




Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), James Msofe, Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini, ambaye pia ni mmoja wa wakufunzi wa masuala ya SDGs, Hoyce Temu na Mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDOM wa Didgrii ya kwanza ya Mifumo ya Upashanaji Habari, Lobezi Kulilo katika picha kumbukumbu wakilishilia mabango ya SDGs.




Baadhi ya wanafunzi wa UDOM walioshiriki semina fupi kuhusu SDGs iliyoandaliwa na ofisi ya Umoja wa Mataifa chuoni hapo katika picha ya pamoja na vibao vyenye Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.




Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa UDOM mara baada ya kumalizika kwa semina kuhusu Malengo ya Dunia iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja Mataifa mjini Dodoma jana.








WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...