Monday, 19 October 2015

UNDP YASISITIZA VITA YA UMASKINI KWA KUTUMIA MAZINGIRA



Mkurugenzi Msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) Tanzania, (Ushauri na Miradi), Amon Manyama akitoa maelezo kuhusu mradi wa PEI na salamu kutoka UNDP kwa washiriki wa mafunzo hayo hivi karibuni jijini Mwanza.

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

MKURUGENZI Msaidizi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Amon Manyama, alisema vita dhidi ya umaskini inakuwa na maana kubwa kama inalinganishwa na mazingira.

Alisema kwamba umaskini wa kipato ambao umekuwa ukipiganwa sana kwa sasa unastahili kupiganwa kwa kuangalia umaskini kutokana na ukweli kuwa kuboreshwa kwa mazingira ndio hatua kubwa ya kupigana na umaskini katika sura zote zilizobaki.

Mkurugenzi msaidizi huyo alisema hayo hivi karibuni mjini Mwanza wakati akielezea mradi wa mtaji na elimu wa UNDP ambao umefanyiwa kazi kwa pamoja kati ya shirika hilo, Tume ya Mipango, Hazina na Ofisi ya Makamu wa Rais, katika mafunzo ya siku moja ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, yaliyofanyika Mwanza.

Mradi huo umelenga kuwezesha ushirika wa akiba na mikopo katika wilaya sita nchini kuwezesha wananchi kushiriki katika kukabili umaskini unaosababishwa na mazingira.

Akifafanua alisema kwamba inawezekana muda wa kusubiri kuvuna samaki ziwani umekwisha kwa hiyo kinachotakiwa kufanyika ni kupanda samaki ndani au nje ya ziwa na watu waweze kutumia nafasi hiyo kuboresha maisha yao.


Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk.Tausi Kida akitoa maelezo ya utangulizi juu ya madhumuni ya mafunzo hayo kwa washiriki kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.

Alisema hali hiyo pia ipo katika misitu. Wakati watu wanakata misitu unawapa elimu na mtaji wa kupanda misitu mingine na hivyo mazingira yakaendelea kubaki na kuwa mtaji wa kukabili umaskini.

Mradi huo ambao upo katika wilaya sita kwa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2021 na ifikapo muda huo utakuwaupo wilaya 21 na kutumika kama kichochea cha utekelezaji wa malengo 17 ya maendeleo endelevu yenye nia ya kupiga vita umaskini, kuondoa ubaguzi na njaa.

Alisema mafunzo yaliyotolewa katika kongamano la viongozi mbalimbali wa vyama vya ushirika vya aina mbalimbali mjini Mwanza kwa msaada wa UNDP na kutekelezwa na Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii (ESRF) yamelenga kuwezesha SACCOS kutambua fursa hizo za mazingira kukabili umaskini.

Alisema katika mazingira ya sasa wanawake ndio wanaathirika zaidi katika umaskini kutokana na wao kuwa wazazlishaji na wahudumiaji wa kaya na kwamba kama kutakuwepo na mabadiliko na mazingira yakatengeneza fursa ya kupiga vita umasikini wanawake wataendelea kustawi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utafiti wa masuala ya kiuchumi na kijamii (ESRF) ESRF Dk. Tausi Kida alisema lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha ushirika wa akiba na mikopo mkoani Mwanza.

Akizungumzia historia ya mradi alisema wao kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) pamoja Tume ya mipango, walianza kutekeleza mradi wa kukuza uchumi, kuleta maendeleo endelevu kupitia utunzaji mazingira, usawa wa kijinsia na kupunguza na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yaani (PEI) toka mwaka 2014.


Pichani juu na chini ni baadhi ya Viongozi wa Vyama vya Ushirika (SACCOS na VICOBA) na Maafisa Ushirika wa kutoka Wilaya za Bunda, Bukoba na Sengerema wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa.

Alisema tafiti mbili chini ya mradi wa PEI zilizofanyika katika wilaya za Bunda, Ileje, Sengerema, Bukoba vijijini, Ikungi na Nyasa kubaini changamoto na fursa zinazopatikana katika wilaya hizo.

Alisema matokeo ya tafiti yalionyesha umuhimu wa kuzipa uwezo taasisi za kifedha kama SACCOSS, VICOBA na vikundi mbalimbali vya kifedha kwa kuzijengea uwezo wa kitaaluma na kifedha.

Alisema hata hivyo pamoja na matokeo hayo Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ilitenga na kutoa fungu la fedha na kuipatia benki ya Twiga ili kukopesha kwa riba nafuu kwenye taasisi kama SACCOSS na VICOBA kwa lengo kuu kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi ili waweze kupata fursa ya kukuza mitaji yao na kuwafanya muweze kutekeleza fursa hizi katika maeneo yao.

UN, SMZ KUSHIRIKIANA KUKOMESHA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA



Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda wakati wa ziara fupi ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani humo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja huo tangu kuanzishwa.

Na Mwandishi wetu, Zanzibar.

Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amesema Umoja huo utaendelea kushirikiana na Serikali ya mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kukomesha vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Akizungumza katika ziara ya kutembelea Dawati la jinsia la Wanawake na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda alisema umoja huo umelenga kusaidia uwepo wa utawala wa sheria na wenye kujali haki na utu wa binadamu kupitia mpango mkakati wake uliomo katika malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) kuanzia mwaka 2016 utakosaidia kuondoa vitendo hivyo.

Alieleza kuwa tatizo la udhalilishaji wa kijinsia sio kwa Zanzibar pekee bali ni la kidunia, hivyo umoja wa mataifa(UN) unawajibu kusaidia juhudi za serikali kupambana na tatizo hilo.

“Tushirikiane kwa kila hatua ili kuondosha vitendo hivi kwani ni tatizo na kero kwa jamii ya Zanzibar pia ni miongoni mwa ishara tosha zinazoashiria uvunjifu wa haki za binadamu.”, alisema Rodriguez na kusisitiza kuwa ili kukomesha vitendo hivyo ni kuwepo na utawala wa kisheria utakaotenda haki kwa wale wanaoozalilishwa utu wao.


Aidha Bw. Rodriguez aliyataka madawati ya jinsia kutumia vyombo vya habari kuwaelimisha wananchi kupambana na vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ili kuhakikisha vinapungua ama kuisha kabisa kwa lengo la kujenga jamii yenye uadilifu.

Naye Mtendaji wa Dawati hilo, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma alifafanua kuwa kesi za ubakaji kwa wanawake na watoto zimepungua ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Alisema kwa sasa kuna changamoto ya utoroshwaji na utelekezaji wa watoto kesi ambazo kwa sasa ni nyingi lakini wanaendelea kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ili kuhakikisha zinapungua.

Akizitaja changamoto zilizopo katika dawati hilo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa ushahidi wa kina kwa baadhi ya kesi hivyo kupelekea kuharibu mwenendo mzima wa kesi kutokana na kukosekana uthibitisho.


Mtendaji wa Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya kituo hicho tangu kufunguliwa ikiwa ni mwaka mmoja sasa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) ikiwa ni awamu yake ya pili kutembelea Dawati hilo. Kulia ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.

Alifahamisha kuwa changamoto nyingine ni jamii ya wazanzibar kuwa na tabia ya mukhari (kuoneana haya) hivyo kumaliza kesi kwa njia ya kifamilia bila ya kufuata utaratibu wa kisheria, hali inayokuwa kikwazo cha kuwafikisha katika vyombo vya kisheria wahalifu wa kesi za ubakaji.

“Bado nasisitiza ni lazima Wazanzibar tubadilike na kuondokana na masuala ya muhari kwani unawaumiza watoto wetu na tujenge utamaduni wa kujiamini kwa kutoa ushahidi ili tutokomeze janga hili.,” alisisitiza Fatma.

Pamoja na hayo alishukru msaada unaoendelea kutolewa na Umoja wa mataifa (UN) kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwawezesha katika mambo mbali mbali kwa lengo la kupunguza vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia.

Mwakilishi huyo Mkazi katika ziara hiyo alitembelea miradi mbali mbali ya umoja huo ikiwa ni moja ya sherehe za kutimiza miaka 70 ya kuanzishwa kwa umoja huo.


Baadhi ya waandishi wa habari wa visiwani Zanzibar na maofisa wa Umoja wa Mataifa waliombatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) katika ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa visiwani humo.


Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipitia kitabu cha orodha za kesi katika Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda. Kulia ni Mtendaji wa Dawati hilo, kutoka Jeshi la Polisi Koplo, Fatma Juma na kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.



Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa ndani ya chumba cha dawati la Jinsia.







Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa Upelelezi wa Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kombo Khamis Kombo (kulia) alipofanya ziara ya kutembelea Dawati la Jinsia na Watoto, Mkoa wa Kaskazini Unguja katika Kijiji cha Mahonda ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za miaka 70 ya Umoja wa Mataifa tangu kuanzishwa. Kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya ulinzi kwa watoto wa UNICEF Zanzibar, Bw. Ahmed Ali.


Mradi huu ulifadhiliwa kwa pamoja kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) na Shirika linalohudumia watoto duniani, UNICEF.


Muonekano wa jengo la Dawati la Jinsia na Watoto mkoa wa Kaskazini Unguja.


MAGZAETI LEO JUMANNE



MKUTANO WA TUME NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA...!


Kamishna wa tume ya uchaguzi ya taifa Jaji (Mst) Mary Longway (katikati) akitoa hotuba wakati wa mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa leo mjini Iringa. Mkutano huo ulikuwa wa kujadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ya uchaguzi na pia kupeana taarifa kuhusu maandalizi ya Uchaguzi Mkuu hapo tarehe 25 Oktoba 2015. Kutoka kushoto walioketi ni Afisa wa tume ya uchaguzi ya taifa William Kitebi na mratibu wa uchaguzi mkoa wa iringa, Wilfred Muyuyu.



Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Iringa Mustafa Msovela akiuliza swali tume kuhusu mgongano wa matamko kati ya viongozi wa siasa na tume juu ya kusimama mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura pamoja na kulinda kura baada ya kupiga kura wakati wa mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa leo mjini Iringa. 


Katibu Mkuu wa CHAUSTA -Taifa Mwaka Lameck Mgimwa akiuliza swali kuhusu utata wa wanavyuo kupiga kura ya urais pamoja na wale waliohama baada ya zoezi la uhakiki la dafatri la wapiga kura wakati wa mkutano wa tume na viongozi wa vyama vya siasa leo mjini Iringa. 








WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...