Tuesday, 13 October 2015

MDAHALO WA WAZI JUU YA AMANI KATIKA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI MKUU

Afisa habari wa Iringa Civil Society Organization (ICISO) Charles Lwabulala (kulia) akimkaribisha mgeni rasmi ambaye ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Selemani Mzee  ili afungue mdahalo wa wazi juu ya amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu unaofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria mjini Iringa. Mdahalo huo umeandaliwa na Iringa civil society organization (ICISO-Umbrella) kwa kushirikiana na The Foundation for civil society

Kaimu wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Selemani Mzee (katikati) ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kilolo akifungua mdahalo wa wazi juu ya amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu unaofanyika katika ukumbi wa chuo Kikuu Huria (OUT)mjini Iringa. Kutoka kushoto walioketi na Katibu Tawala wa Wilaya ya Kilolo Martin Mlwafu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi, Mwenyekiti wa ICISO Alexander Kisinini na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Iringa, Wilfred Myuyu na Afisa Habari wa Iringa Civil Society Organization (ICISO) Charles Lwabulala . Mdahalo huo uliandaliwa na Iringa Civil Society Organization (ICISO-Umbrella) kwa kushirikiana na Asasi ya Foundation for Civil Society (FCS)leo. (Picha na Friday Simbaya)





Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akitoa mada kuhusu amani na usalama wakati wa mdahalo wa wazi juu ya amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu unaofanyika katika ukumbi wa chuo kukuu huria mjini Iringa. Mdahalo huo umeandaliwa na Iringa civil society organization (ICISO-Umbrella) kwa kushirikiana na The Foundation for civil society. (Picha na Friday Simbaya)




No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...