Thursday, 18 June 2015

PROFESA MARK MWANDOSYA AENDELEA KUSAKA WADHAMINI MKOANI IRINGA

Waziri na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profsea Mark James Mwandosya akisalimiana na wanachama na wadhamini baada ya kutoka katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijini leo.

 


Waziri na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profsea Mark James Mwandosya akiondoka kutoka katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijini leo baada ya kupata wadhamini na kuelekea Uwanja wa ndege Nduli kwa ajili ya safari ya kwnda mkoani Tabora.


Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Hakimu Jackson (kushoto) akimkabidhi fomu ya majina ya wadhamini Waziri na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profsea Mark James Mwandosya katika Ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijini leo. (Picha Na Friday Simbaya)




Waziri na Mbunge wa Rungwe Mashariki, Profsea Mark James Mwandosya aendelea kusaka wadhamini mkoani Iringa ili apewe ridhaa ya kupeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.

Profesa Mwandosya alisema kuwa endapo atapata bahati ya kupeperusha bendera ya chama chake katika mbio za kuwania urais mwaka huu na kufanyikiwa kushinda urais, atahakikisha elimu afya, ajira kwa vjiana inaboreshwa pamoja na kuboresha huduma za afya kwa wazee.

Profesa Mwanadosya ambaye aliongozana na mke wake Mama Lucy Mwandosya wafika tangu juzi mjini Iringa kusaka wadhamini pamoja na kuongea nao.

Wadhimini waliotoka sehemu mbalimbali walifika katika ofisi kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Vijijijni ambapo hata hivyo alipata wadhamini zaidi ya 36 katika mbio za kusaka urais.

Profesa Mawandosya pamoja timu yake wameondoka nkoani Iringa kuelekea mkoani Tabora kuenelea na kazi ya kutafuta wadhamini baada ya kuzunguka zaidi ya mikoa mitano mpaka sasa.


Idadi ya wagombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inazidi kuongezeka na kwa sasa kufikia wagombea 36.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...