Na Gustav Chahe, Tanga
Kiwanda cha uzalishashi
maziwa “Tanga Fresh Limited” kilichopo Mkoani Tanga kinakabiliwa na
changamoto ya upungufu wa zao la maziwa hali inayotokana na ukosefu wa malisho
kwa ng’ombe hasa kipindi hiki cha kianzazi.
Akiongea na mwandishi wa
habari hizi kiwandani hapo hivi karibuni, afisa habari wa kiwanda hicho Bw.
Charles Tumaini ameeleza kuwa kwa sasa kiwanda hicho kinalazimika kujiendesha
kwa hasara kutokana na kushindwa kufikia asilimia 100 ya uzalishaji kulingana
na nguvu ya mitambo iliyopo.
“Kwa sasa uzalishaji ni
asilimia 60 tu ambayo sawa na lita 50,000 tu kwa masaa 8, hatujafikia kiwango
cha asilimia 100 ya uzalishaji kulingana na nguvu ya mitambo yetu; kwa sasa
tunazalisha asilimia 60 tu ambayo sawa na lita 50,000 kwa muda wa masaa 8 kila
siku” alisema Bw. Tumaini.
“Tunakabiliwa na
changamoto mbalimbali ambazo zinatukwamisha kuzalisha maziwa kwa wingi ambazo
miongoni mwake ni kukosa malisho, maji ya kutosha na kukosa chakula cha kutosha
kwa wanyama wetu” alisema Bw. Tumaini.
Mbali na kiwanda kukosa
uwezo wa kusambaza chakula kwa wafugaji wao, baadhi ya wafugaji wenyewe
wamekuwa wakishawishwa na bei za mitaani na kuuza maziwa yao huko na kiwanda
kukosa maziwa yakutosha.
“Baadhi ya wafugaji
wamekuwa wakishawishwa na bei za mitaani na kuuza maziwa yao huko huku kiwanda
kikiwa kikikosa maziwa ya kutosha” alisema.
Lita moja ya maziwa
kiwandani hapo hununuliwa kwa shilingi 528 wakati mitaani watu hununu kwa
shilingi 1,000 mara mbili ya bei ya kiwandani.
Licha ya wafugaji wengi
kuuza maziwa yao mitaani, wengi wao hawana mafunzo ya ufugaji na kushindwa
kuzalisha maziwa yenye kiwango na kuiomba serikali kutoa mafunzo kwa wafugaji
kupitia maofisa ugani waliopo pamoja na kuongeza idadi yao ili kuweza kuboresha
ufuji.
“Wafugaji wengi wanakosa
mafunzo na kushindwa kuzalisha maziwa yenye kiwango. Hivyo, tunaiomba serikali
katika kilimo kwanza wawafikirie wafugaji ili nao wapewe kipaumbele hasa katika
kuwapa mafunzo. Pia maofisa ugani waendelezwe na wapewe mafunzo ya kutosha ili
waweze kuwahudumia wafugaji na kuboresha ufugaji wao” alisema.
Serikali imeombwa
kuingilia ili kuwepo na mpango endelevu wa kupata maziwa mazuri yakutosha kwa
ajili ya uzalishaji kiwandani hapo ikiwa ni pamoja na kuweka mpango
endelevu wa uthibiti wa magonja ya mifugo.
“Tunaiomba hata serikali
iingilie ili tuweze kupata maziwa mazuri; wakati mwingine inatokana na
kutokuwepo mpango maalumu wa uthibiti wa magonjwa ya wanyama. Hivyo, tunaomba
uwepo mpango endelevu wa uthibiti wa magonjwa hayo ili uzalishaji wa maziwa
uweze kuongezeka kila siku vinginevyo tutapoteza uzalishaji wetu na kipato”
alisema.
Bw. Tumaini amewaomba
wafugaji kutokukata tama katika kipindi hiki na kuendelea kupeleka maziwa
kiwandani hapo bila kujali changamoto zinazojitokeza.
MWISHO
No comments:
Post a Comment