Friday, 20 March 2015

POLISI WAMALIZA MZOZO WA TUNDUMA


JESHI la Polisi mkoa wa Mbeya, limefanikiwa kuzima mzozo na vurugu zilizodumu kwa siku tatu eneo la Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya.

Vurugu hizo zilitokea baada ya kiongozi wa Mtaa wa Makambini kata ya Sogea (chadema) kuwadanganya baadhi ya wananchi anaowaongoza kuwa alikuwa ameshinda kesi ya kiwanja kinachomilikiwa na Chama Cha Mapinduzi(CCM), na kuamuru uchimbwe msingi ili ijengwe hospitali.

Baada ya hali hiyo kujitokeza, baadhi ya viongozi wa CCM walitoa taarifa Polisi ambapo pande mbili ziliitwa na kusikilizwa ambapo kesho yake Machi 15, mwaka huu, kiongozi wa Chadema alikwenda katika eneo hilo akiwa na wafuasi wake kwa ajili ya kuchimba msingi wa hospitali hiyo.


Wanachadema hao walitaka kujenga hospitali hiyo bila kuzingatia taratibu karibu taratibu zote ikiwa ni pamoja na kutokuwa na ramani na kutofahamu kuwa hospitali haijengwi ngazi ya mtaa.
 
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Mbeya, Kamanda wa Polisi Ahmed Msangi, amesema kuwa walipofika Polisi kuwasimamisha wasiendelee na zoezi hiyo, wakaanza kurusha mawe na walipojaribu kuwatawanywa, wakaanza kuchoma matairi katikati ya barabara na kuzua tafrani zaidi.

Alipoulizwa kwanini jeshi lake lilitumia nguvu kubwa kudhibiti ghasia hizo, Msangi alisema kuwa nguvu iliyotumika ni ya kawaida na ilitumika kutokana na tukio lenyewe lilivyokuwa.



“Nguvu ilikuwa ya kawaida na ndio iliyotumika kumaliza ghasi hizo zilizokuwa zikifanywa na wahuni pamoja na viongozi wa kisiasa,” alisema.
CHANZO;KALULUNGA MEDIA

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...