Wednesday, 7 May 2014

ZITTO KABWE AGEUKA KIVUTIO MAZISHI YA BABAKE FILIKUNJOMBE LUDEWA

Kutoka  kushoto mkuu wa wilaya ya  Ludewa  Juma Madah ,mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe na mbunge wa jimbo la  kigoma kaskazani Zitto Kabwe wakiwa katika msiba wa babake Filikunjombe mjini Ludewa jana.


DC Ludewa Bw Juma Madaha akitambulisha  viongozi mbali mbali




Mbunge wa  jimbo la Ludewa  Deo Filikunjombe kushoto  akilitazama jeneza lenye mwili wa babake marehemu  Frolian Filikunjombe likiingizwa  ndani ya kanisa la RC Ludewa kwa ajili ya ibada ya mwisho kabla ya mazishi  yaliyofanyika katika makaburi ya Ludewa mjini


Na Francis Godwin Blog 
MBUNGE  wa  jimbo la Kigoma Kasikazin Zitto (CHADEMleo amegeuka  kuwa  kivutio  kikubwa  katika mazishi ya babake mbunge wa  jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe huku wananchi  wa  jimbo  hilo na viongozi wa CCM mkoa  wa Njombe  wakimbebesha majukumu  ya ubovu wa barabara  kwa  kumtaka  kushirikiana na mbunge wao  kuwasha moto bungeni .
Zitto  ambae  katika msafara  wake  huo  aliongozana na mbunge wa  jimbo la Mwibara Kangi  Lugola (CCM) mbunge wa  viti maalum mkoa wa  Tanga Amina Mwidau (CUF) na  wengine wa CCM nusuru avuruge  msiba  huo baada ya  wananchi  kuonyesha  kuvutiwa na uwepo  wake na  kumtaka   kusikia  sauti  yake .
Awali  wakati wa utambulisho  wa  viongozi wa kitaifa  uliofanywa na mkuu wa  wilaya ya   Ludewa Juma Madaha  waombolezaji  baada ya  kusikia  jina la Zitto Kabwe  katika orodha ya wabunge hao ndipo  sauti  ziliposikika  kuwa  wanahitaji azungumze .
Hata hivyo  katika  salam  zake katibu wa itikadi na uenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya mbali ya  kumpongeza  mbunge Kabwe kwa  kufika katika msiba   huo na timu  yake bado  alimtaka  Kabwe na timu  yake  kusaidiana na mbunge  wao Filikunjombe kupigania ujenzi wa barabara ya lami kati ya Ludewa na Njombe.
"Mheshimiwa  Zitto Kabwe wewe ni mmoja kati ya wapiganaji wa kweli  bungeni kama  alivyo mbunge  wetu na jembe  letu wana Ludewa  Deo Filikunjombe ....sasa tunaamini mmeona ubovu wa barabara ya Njombe - Ludewa hivyo  kupitia ninyi  sisi  wana Njombe na Ludewa  tunaomba msaidiane na Filikunjombe kupigania suala la ubovu wa barabara na sio  kutoka nje ya bunge pindi suala la ubovu wa  miundo mbinu linapotolewa na mbunge  wetu"
Kufuatia  ombi hilo la Mgaya  waombolezaji walilipuka kwa  furaha   huku Zitto  Kabwe  akionyesha kuguswa na ombi hilo na kumtania mbunge wa  viti maalum mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF)  kuwa UKAWA hao .
Zitto Kabwe  ambae alikuwa ni mmoja wa abiria  waliosafiri pamoja na babake Filikunjombe mzee Frolian Filikunjombe kabla ya kufariki  dunia akiwa  ndani ya ndege  kutoka  Dubai kuja nchini ni  mmoja  wa   marafiki  wakubwa wa mbunge Filikunjombe na pia ni mwenyekiti wa kamati ya PAC ambapo  Filikunjombe ni makamu mwenyekiti wake.
Hata  hivyo  alisema  kuwa  ombi la  wana Ludewa  kwake atalifanyia kazi na  kuwa suala la siasa lina  sehemu yake na yanapozungumzwa mambo ya kimaendeleo siasa  za  vyama zinawekwa kando .
Hivyo  alisema  kuwa kutokana na mahusiano mema  kati yake ya mbunge Filikunjombe ameguswa na msiba  huo na kuwa pindi atakapofika  bungeni maombi ya  wana Ludewa atayatendea kazi . (FS)


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...