LUDEWA
WANANCHI Wilayan ya Ludewa mkoani Iringa wako hatarini kugeuka wakimbizi katika siku za usoni kutokana na hofu ya maeneo yao kugawiwa kinyemela na ofisi za madini kanda zilizoko mkoani Mbeya imefahamika.
Hofu na mashaka vilitanda hivi karibuni kwa madiwani wote walipotembelea katika Kata ya Iwela ambako kulikuwa na wasiwasi miongoni mwa wananchi waishio katika maeneo hayokuwa baadhi ya wachimbaji wageni wenye mitambo wasio na vibali wameingia na kuvamia kwa kuanza shughuli za uchimbaji bila wananchi kujulishwa.
Katika Baraza la Madiwani (Full Council) madiwani katika halmashauri hiyo waliitaka Wizara ya Nishati na Madini kutumia busara na uungwana kuhusu suala la ugawaji maeneo kwa sababu pamoja na kuwepo Sheria za Madini, lakini wananchi nao wanayo haki ya kusikilizwa na kuhusishwa ili kuepusha migongano ya baadaye.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Matei Felician Kongo akizungumza katika baraza hilo alioneshwa kusikitishwa kwake kusikia kila eneo ndani ya wilaya limetolewa kibali bila wananchi kujulishwa kwa kufanya hivyo usalama wa wanaLudewa huko wapi kama eneo lote limejaa vibali? Aliuliza Bw. Kongo huku akimwagiza mkurugenzi kufuatilia.
Kwa upande wake Bi. Hilda Lauwo ambayo ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ludewa alisema ni hatari sana kama wananchi hawaelewi kama maeneo yao ya makazi yamegawiwa kinyemela na kwamba watakapokuja kujua na kutakiwa kuondoka itatuletea matatizo na hasara kubwa kwa sababu uzoefu umeonekana katika maeneo ya wenzetu.
Bi. Lauwo alisema tumeona matukio mengi ya mauaji huko kwenye maeneo ya madini na kuongeza kuwa kuna haja ya kufuatilia jambo hili kwa wahusika ili kujua mstakabali wa wilaya, hatutaki yaje yatukute na sisi baadaye.
“Kama hatutapata ufumbuzi wa hili tatizo mapema tutakuja kupata shida kubwa baadaye, hivyo ni vema kamishna wa madini kanda aje atueleze na wananchi waelewe mapema kabisa kabla haya mambo hayajakuwa magumu,”alisisitiza Bi. Lauwo.
Aliongeza kuwa bila kufanya hivyo hii Wilaya ya Ludewa itakuja kuwa na matatizo kuliko wilaya zingine kwa hiyo ni vizuri wananchi wakaambiwa na kujulishwa maeneo yote yaliyokwisha kugawiwa na pengine kamishna aeleze ni vigezo gani alitumia kugawa maeneo yote ya Wilaya hii bila taarifa na inasemekana hadi sasa kuna vibali 70 vimeshatolewa.

No comments:
Post a Comment