MHANDISI WA MAJI LUDEWA ASHANGAZA KWA KUACHA FAMILIA NA KUKESHA ENEO LA MRADI KUHAKIKISHA WANANCHI WANAPATA MAJI SALAMA NA KWA WAKATI.
WANANCHI katika Kata za Manda, Luilo na Masasi katika Tarafa ya Masasi Ludewa, mkoani Iringa wameiomba serikali kuongeza nguvu zaidi katika mradi wa maji uliokuwa umeshindikana muda mrefu ama kwa kukosa rasilimali wataalamu wenye uwezo au fedha ili kuweza kufikisha maji katika maeneo yaliyobaki baada ya Bw. Christopher Nyandiga (Mhandisi wa Maji wilayani humo) kufauru kufikisha maji katika baadhi ya maeneo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wadau, wananchi na watumiaji wa maji hayo hawakusita kumshukuru na kumpongeza mhandisi wa maji wilayani humo Bw. Christopher Nyandiga na kumtaja kama mkombozi wa maisha yao kwa kuwa ni miaka mingi maji ya bomba yamekuwa ndoto kwao kutokana na ukilitimba wa wataalam na wahandisi waliotangulia.
“Mradi wa maji katika Tarafa yetu ya Masasi una historia ya ajabu kuna wakati katika miaka ya themanini, Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi aliitwa kuja kuzindua tanki la maji kumdanganya kuwa maji hayo yametokana na bomba kumbe waliyachota ziwa nyasa na kuyajaza na baada ya kuzindua tu ukawa ndiyo mwisho,” alisema mmoja kwa masharti ya kutoandikwa jina gazetini.
Alisema wananchi wana kila sababu ya kuishukuru Halmashauri ya Wilaya kwa kusikia kilio chao, lakini pia kwa kuwapelekea mhandisi mbunifu, mwenye uwezo kitaaluma, lakini mwenye kujituma kwani hawajawahi kuona mtaalam kuacha familia yake na kuhamia katika eneo la mradi huku yeye mwenyewe akifanya kazi kama fundi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa Bw. Matei Felician Kongo akizungumza katika eneo la mradi alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri Bi. Hilda Lauo kwa uwamuzi alioufanya hasa Mhandisi wa Maji Wilaya ya Ludewa Bw. Christopher Ndindiga kwa kuvua cheo chake na kuhamia eneo la mradi hadi ulipokamilika.
“Mradi huu si wa leo ni wa muda mrefu sasa ni zaidi ya miaka ishirini, awali ulikuwa ukiitwa Lifua- Manda Project wakati huo kulikuwa na ugonjwa wa kipindupindu huku ukilenga kupeleka maji hayo katika Sekondari ya Manda,” alisema Bw. Kongo huku akifurahia mafanikio.
Bw. Kongo alisema katika miaka ya 1979 hadi 1980 mradi huo ulikuwa unategemea chanzo cha mto Kilumbila ambao sasa unaendeshwa na wamisionari, hata hivyo hakuwa na uhakika kama ni shilingi ngapi zilitumika katika miradi hiyo kwani ni muda mrefu sasa.
Mradi huu mpya chanzo chake ni mto Mchuchuma ambao unayomaji ya kutosha na unahudumia kwa sasa katika vijiji vya Luilo, Lihagule, Manda na Masasi, hata hivyo mradi wenyewe umekuwa wa kuungaunga hii ni kutokana na fedha kutofika kwa wakati na wakati mwingine kuwa kidogo.
Bi. Winfrida Kilumbo (Kizota) Diwani wa Kata ya Manda kwa upande wake alimshukuru na kumpongeza Mhandisi wa Maji, Bw. Christopher Nyandiga kwa moyo wa kizalendo kwani aligeuka kuwa fundi yeye mwenyewe na kuuweka uhandisi pembeni.
Kizota alisema Wananchi wa Manda wamekuwa wakitumia maji ya Ziwa Nyasa ambayo kwa kipindi cha masika si salama. Lakini mradi huu ni ukombozi mkubwa kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Manda na walimu kwani wamekuwa wakitegemea maji ya ziwa yanayopatikana umbali wa zaidi ya kilomita tano.
“Wanafunzi wamekuwa wakibeba maji kichwani kwa matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na walimu wao kila siku wanapokwenda shuleni kwa kipindi chote cha miaka mine, lakini tunashukuru sasa tatizo hili limekwisha baada ya maji kufika shuleni hata ujenzi wa majengo umerahisishwa,” alisema Bi. Kizota.
Kwa upande wake, mhandisi wa maji wilayani Ludewa Bw. Nyandiga alisema alilazimika kufanya hivyo kutokana na shida wanayoipata wananchi wa Tarafa ya Masasi kwa muda mrefu sasa na kwamba amefanikiwa kuyafikisha maji katika baadhi ya maeneo machache na kwamba sehemu zingine zitaendelea kupata kadri ya upatikanaji wa fedha, lakini akawataka wananchi kutunza na kuyalinda mabomba hayo ili yaweze kuwatunza.

No comments:
Post a Comment