Mwanahabari Frank Kibiki (wa pili kutoka kulia) akibadilishana mawazo na wanahabari wenzako jana walipokutana katika jengo la NSSF-Akiba House ambapo karibu na ofisi za nipashe na majira. |
MWANAHABARI FRANK KIBIKI ambaye pia nimtangaza nia ya ubunge katika Jimbo la Jringa mjini kupitia tiketi ya CCM amewataka wakinamama kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
MWANAHABARI FRANK KIBIKI ameeleza kuwa wanawake waondoe hofu ya kugombea hasa kukiwa na ushindani wa wagombea wanaume kwa kuogopa kuchafuliwa kwa mambo yasiyokuwepo.
Ameendelea kusema kuwa wananchi wasishawishiwe na propaganda za wanasiasa na badala yake wachague viongozi bora wenye uwezo wa kuongoza kutoka katika chama chochote.
Aidha ameongeza kuwa viongozi wawe na sera za kutekelezeka ili kuwatendea haki wapiga kura wao hali itakayowafanya waaminike katika jamii.
Mbali na hayo MWANAHABARI FRANK KIBIKI amewakumbusha vijana kutokubali kutumiwa na baadhi ya wanasiasa katika kuleta vurugu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu na badala yake wachague kiongozi mwenye weredi na sifa za kuwa kiongozi kutokana na sera za chama chake.
No comments:
Post a Comment