Sunday, 26 June 2011

MWENYEKITI TLP SONGEA AFARIKI DUNIA


Na Friday Simbaya,
S ongea
PAROKO Padre Joseph Ndimbo wa Parokia ya Peramiho Jimbo Kuu la Songea aliwaasa  waombolezaji kuacha mara moja tabia kugombeana maeneo ya kuzika marehemu.
Alisema kuwa kuna mtindo umezuka wanandugu kuvutana wapi wamzike marehemu na kuongeza kuwa huku ni kumdhalilisha marehemu.
Pd. Ndimbo alisema hayo Jumamosi wakati wa mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Tanzania labour Party (TLP)wilaya ya Songea, Bw. Kalo Kombe katika makaburi ya Liangano karibu na Kijiji cha Lipinyapinya Kata ya Peramiho.
Alisema kuwa sio tabia nzuri kwa wanandugu kugombeana maiti , kumbe maeneo yote yanafaa kuzikia.
“Imezuka tabia katika jamii ya watu kugombania maiti yaani mvutanao wa watu wawili kugombania maiti wakati wa  mazishi kila mtu anataka kuzika mahali pake, huku kote ni kuhangaika na kumtesa marehemu. Kuzikwa ni kuzikwa tu hata kama atazikwa Peramiho ‘A’ au Peramiho ‘B’,” alitoa mfano paroko huyu.
Aidha, paroko alisisitiza kuwa watu wasitafute mchawi kwamba marehemu amerogwa bali waendelee kumuonbea marehemu kuwa astarehe kwa amani kwa Mungu Baba.
Aliwaambia waombolezaji kuwa kuumwa kwa mwanadamu ni mateso kwa sababu mtu yeyote atakayependa maisha lazima afe lakini anayechukia maisha ataishi maisha ya milele.
Aliongeza kuwa WaTanzania vilevile tunakiwa  kufanya kazi kwa bidii sio kutafuta kwa njia ya mkato. Alisema kuwa mtu lazima apate mateso ili afe kama vile mtu anatakiwa kuteseka ili apate chakula. Aliongeza kuwa mateso ni sehemu ya maisha ya binadamu, kwa hiyo mtu akiuugua ni mateso, vilevile mtu kuchapakazi kwa bidii ni mateso pia ili kuweza kuishi maisha bora.
“Hakuna maisha bora kama hujishughulishi kwa sababu maisha bora huja kwa kufanyakazi kwa bidii na kuaacha uvivu,” alisema paroko. “Asiyefanya kazi na asile huo ndio wito wangu kwenu” alisisitiza.
Mwenyekiti huyo wa TLP  alifariki dunia juzi katika hospitali ya Misioni ya St. Joseph Peramiho baada ya kuugua vidonda vya tumbo kwa muda mrefu.
Marehemu Kombe alistaafu katika Jeshi la Polisi tangu 1995, ambapo alifikia renki ya inspector kabla ya kustaafu na kuanza kujishughulisha na mambo ya siasa. Marehemu Kombe alipenda magauzi ndiyo maana alijiunga na upinzani, alikuwa anaishi maeneo ya Mjimwema katika Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...