Monday, 20 June 2011

MTOTO ANUSURIKA KUUNGUA MOTO


Mafundi wakiendelea na ukrabati wa nyumba iliyoteketea kwa moto hivi karibuni maeneo ya Peramiho, ambapo mtoto mdogo anayesoma shule ya chekechea alinusurika kuungua moto na baadae kuokolewa na wasamaria wema kwa kubomoa mlango kwa shoka. Mtoto huyo mara baada ya kuokolewa alikimbizwa katika hospitali ya Peramiho kwa uchunguzi zaidi, baada kubugia moshi mwingi. Mashuhuda waliongea na mwandishi walisema kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyosababishwa na jiko la umeme lililoaachwa bila uwanagalizi. Aidha, familia mbili ambazo zilikuwa zikiishi katika nyumba hiyo kwa sasa zinajistili kwa majirani kwa muda huu huku wakisubiri kumalizika kwa ukarabati wa nyumba kwa kwekuweka bati badala ya vigae vilivyokuwa hapo mwanzo.




Fundi mmoja  akitoa mabaki  mbalimbali ya vyombo vya ndani kutoka chumba kulichonzia kuungua moto.


No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...