Wednesday, 29 April 2015

FANYENI REDIO ZENU ZITAMANIKE, WAMILIKI REDIO JAMII WAAMBIWA


Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Bw. Ramadhan Ahungu akiendesha mafunzo ya masoko na mpango biashara kwa viongozi wa redio jamii nchini wakati kuhitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano iliyoratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ambayo imefanyika katika kituo cha Redio jamii Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.


Na Mwandishi wetu, Mwanza


WAMILIKI wa redio za jamii wametakiwa kujenga taswira njema za redio zao ikiwa wanataka redio zao zitamanike na kutumiwa na wadua mbalimbali wa maendeleo nchini.


Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu.


Akizungumzia malengo ya warsha hiyo na madhumuni yake alisema kwamba kuwapo kwa mpango wa biashara ndani ya redio hizo hakutakuwa na maana kama wasipozingatia ujenzi wa taswira utakaowafanya wadau kuvutiwa na redio hizo.


Alisema kuna umuhimu wa suala hilo kwani kusipojengeka kwa mahusiano bora kati yake na jamii, watu binafsi na taasisi za kiraia zenye malengo tofauti katika kuhudumia wananchi, redio hizo hazitakuwa na biashara ya kufanya.


Ahungu pamoja na kusifia mtindo uliotumika kuwezesha redio hizo kuandaa mipango kazi ya biashara yenye lengo la kusimamia masoko na fedha alisema warsha imefanikiwa kuwaweka karibu zaidi na wadau wamiliki wa vyombo hivyo.


Warsha hiyo ni hitimisho ya awamu ya kwanza kwa ufadhili wa mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo redio za jamii katika matumizi ya Tehama na mawasiliano inayoratibiwa na Shirika la Kimataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO iliyofanyika katika kituo redio cha Sengerema Telecentre mkoani Mwanza.


Alisema katika warsha hiyo wamiliki hao walijifunza uandaaji wa mipango ya biashara, kutunza fedha, utafutaji masoko, uhakiki wa mipango ya biashara na vipindi vya redio kwa lengo la kuona namna ya kuvifanya kuleta biashara.


Naye Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa akizungumzia mafunzo hayo alisema yamemsaidia sana katika kuhakikisha kwamba kituo chake kinakuwa bora na kinachovutia watangazaji.


Alisema mafunzo hayo yamewafanya wajitambue kwani yamefanyika mfululizo kwa mara 5 na kuwafanya wabadilike.


Aidha Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula alisema kwamba anashukuru mafunzo kwa kuwa yamewafanya kuondoa mawazo vichwani na kuweka mipango kazi katika karatasi na kuwezesha wafanyakazi nao kufuatilia.


Meneja wa kituo cha Redio Jamii FADECO ya wilayani Karagwe, Adelina Lweramula akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo yaliyomalizika jana kwenye kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.


Meneja wa kituo cha Redio Jamii Kahama FM ya Shinyanga, Marco Mipawa akiuliza swali kwa mkufunzi wa warsha ya mafunzo ya masoko na mpango biashara (hayupo pichani) wakati wa kuhitimisha warsha ya awamu ya kwanza inayofadhiliwa na mradi wa SIDA kwa kushirikiana na UNESCO iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii cha Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.



Pichani juu na chini ni Viongozi wa Redio Jamii nchini walioshiriki mafunzo ya masoko na mpango biashara yanayofadhiliwa na mradi wa Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kuzipa uwezo Redio hizo katika matumizi ya Tehama na Mawasiliano na kuratibiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sayansi na Utamaduni UNESCO ikiwa ni hitimisho la warsha ya awamu ya kwanza ya mradi huo yaliyofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.






Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu akiendelea kuwapiga msasa viongozi hao namna ya kutafuta masoko na kuboresha mpango biashara.

Mwezeshaji wa warsha ya Viongozi wa vituo vya redio jamii Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo na wakati (ASMET), Ramadhan Ahungu (kulia) akibadilishana mawazo na Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al Amin Yusuph (wa pili kulia) wakati wakijiandaa kwa zoezi la picha ya pamoja. Kushoto ni Mshauri na Mkufunzi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Rose Haji Mwalimu akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa vituo vya Redio Jamii nchini.

Picha ya pamoja ya Wakufunzi na washiriki wa warsha ya mafunzo ya masoko na mpango biashara iliyomalizika jana katika kituo cha Redio Jamii Sengerema-Telecentre mkoani Mwanza.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...