Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu amekanusha uvumi unaoenea mkoani hapa
kuwa amesimamishwa uanachama pamoja kuvuliwa nafasi zote za uongozi leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ofisi za Iringa Press Club (IPC).
UTANGULIZI
Mtakumbuka kuwa tarehe 2/3/2015 kuna kauli ambayo ilitolewa na Katibu wa wilaya ya Mufindi Ndugu Mtaturu. Ambayo ilielekeza baadhi wanachama wetu, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa uanachama kwa baadhi ya makada wetu. Akiwemo Shukuru Luhambati, Clara Shirima na Hosea Kaberege. Swala hili limeamusha malalamiko na mjadala miongoni mwa wanaCCM na wapenzi na wakereketwa wa CCM. Kila mtu akiwa na mtizamo wake kuhusu swala hili, ambalo pia kimepelekea kuamsha malumbano katika vyombo mbali mbali vya habari.
Lakini pia kumetokea wasi wasi mkubwa kwa baadhi ya wanachama ambao walihojiwa na kamati za maadili na kuwa na uvumi pia kuwa watafukuzwa au kunyang’anywa uanachama.
Hiyo pia imeleta uvumi kuwa Mimi Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Iringa pia nimesimamishwa uanachama na kuvuliwa nafasi zote za uongozi.
Moja, Sitofahamu iliyojitokeza kwa wale walioachishwa UANACHAMA: (Shukuru Luhambati, Clara Shirima na Hosea Kaberege)
Kwa mujibu wa Kanuni za Uongozi na Maadili za CCM. Toleo la 2010 zilizotolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa. Fungu la Nne (8vi) pg 30 linalohusu adhabu mbali mbali kwa makosa yanayohusu ukiukwaji wa Maadili. Inasema katika kipengele hicho:
(vi) Kuachishwa Uanachama:
MwanaChama anayegundulika ana makosa ya Itikadi, yanayoathiri Uhai wa Chama, au ambaye ameshindwa huko nyuma kujirekebisha hata baada ya Karipio, wala haonyeshi dalili za kuweza kujirekebisha hata akipewa muda zaidi, basi Kamati ya Usalama na Maadili ya Taifa inaweza kupendekeza mbele ya Kamati Kuu mwanachama huyo aachishwe UANACHAMA. Ikiridhika, Kamati Kuu itapeleka shauri hilo mbele ya Halmashauri Kuu ya Taifa kwa uamuzi wa mwisho.
Adhabu ya kuachishwa Uanachama itatangazwa hadharani.
Pia Fungu la Tatu linalohusu: WAJIBU WA KUSIMAMIA TABIA, MWENENDO NA VITENDO VYA MWANACHAMA NA KIONGOZI;
Ni wa vikao vya Chama cha Mapinduzi vya Halmashauri kuu na Kamati zake za Siasa kwa kila ngazi kama ilivyoanishwa kikatiba.
Kwa swala la leo hapa: Ibara ya 93(8), (14) na (15), Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa:-…….(14) Kumwachisha au kumfukuza Uanachama Mwanachama ye yote endapo itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uanachama. Mwanachama anayeachishwa au kufukuzwa uanachama anaweza kukata rufaa kwa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Hivyo basi, hakuna sababu yakuwa na hofu au mashaka. Wale ambao wanadhani hawajatendewa haki wanahaki ya kukataa rufaa vikao vya juu zaidi, kama Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa.
Pili, Kuhusu Mwenyekiti wa CCM Mkoa kusimamishwa Uongozi sio kweli. Ibara 93 (15) fungu la tatu. Halmashauri Kuu ya Mkoa; Inaweza Kumwachisha au Kumfukuza Uongozi kiongozi ye yote ambaye uteuzi wake wa mwisho unafanywa na Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa.
Pia,Ibara 95(7) Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya Mkoa;
Kumsimamisha uongozi kiongozi ye yote wa ngazi ya wilaya endapo itaridhika kwamba tabia na mwenendo wake vinamwondolea sifa za uongozi. Isipokuwa kwamba haitakuwa na uwezo wa kumsimamisha uongozi kiongozi ambaye uteuzi wake wa mwisho haukufanywa na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa.
Kwa nafasi yangu mimi kama Mwenyekiti wa Mkoa siwezi kusimamishwa uongozi na ngazi ya Mkoa. Hata pia kwa nafasi ya Diwani lazima ipelekwe vikao vya ngazi ya Taifa.
Ingawa wilaya ya Iringa Mjini kupitia Katibu wake Zongo Lobe Zongo wamenipa Adhabu mimi Mwenyekiti wa Mkoa kwa Kupewa Adhabu ya Onyo Kali. Taratibu nyingine zitafuatwa kwa mujibu wa vikao.
Nina toa maelekezo pia kwa Kamati za Maadili zote katika ngazi zote za Mkoa wa Iringa kuzingatia kanuni, Katiba na maelekezo ya Chama katika utekelezaji wao wa Kazi zao za Kamati ili kutoviyumbisha vikao vya maauzi vya Chama. Pia ili kuondoa mgongano unaweza ukajitokeza kati ya viongozi, wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla wake. Kwa mujibu wa Kanuni za uongozi na maadili toleo la 2012; fungu la nne 7(1)…”Katika kusimamia maadili ya viongozi wa CCM wakati wo wote wa utekelezaji wa kanuni hizi, ..Kamati ya Usalama na maadili katika ngazi inayohusika (mkoa) itazingatia Katiba ya CCM na Kanuni zingine za CCM zitakazo kuwepo wakati huo, pamoja na maelekezo mengine ya msingi yatakayokuwa yametolewa na Halmashauri Kuu ya Taifa”.
Ninawasisitiza kuzingatia zaidi; Kanuni za Uongozi na Maadili fungu la Nne 7(4)ii-kinachohusu Tuhuma: Kinasema
”Uchambuzi wa tuhuma hizo utafanywa kwa kutumia njia mbali mbali pamoja na mashahidi watakaoweza kupatikana.
Na endapo itadhihirika kwamba tuhuma zina uzito, mtuhumiwa atatitwa mbele ya kikao cah Kamati ya Usalama na Maadili ya ngazi inayohusika, kama ni lazima, ili apate kuhojiwa ana kwa na.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa
Madam Jesca Msambatavangu
No comments:
Post a Comment