Na Friday Simbaya, Iringa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa katika kukabiliana na ajali za barabara limeanza kufanya operesheni ya kukagua leseni za madereva wote wa magari yakiwemo mabasi ya abira.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa, Juma Bwire alisema kuwa kutokana na kuwepo na leseni za kugushi pamoja na kukosekana kwa mafunzo kazini kwa madereva. Alisema kuwa mafunzo hayo ni ya kukumbushana
Kamanda Bwire alisema kuwa operesheni hiyo itaanza Julai 4 hadi Julai 7 mwaka huu, ambapo tarehe 9 Julai hadi Jumamosi ya Julai 14 wanatarajia madereva kwa lengo la kuwapatia mafunzo kazini.
Hatua hiyo imekuja kufuatia mabadiliko ya mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP) Simon Sirro kufanya mabadiliko ya makanada wa polisi katika baadhi ya mikoa.
Mabadiliko hayo kwa mujibu wa IGP ni kwa lengo la kuoongeza juhudi za kuzuia ajali zinazotokana mara kwa mara katika baadhi ya mikoa.
Kwa upande wake, Salum Chang’a ambaye ni dereva wa mabasi Nani kaona aliponza jeshi la polisi kwa operesheni hiyo na kuwaoba madereva wenzake kutoa ushirikiano katika kukabiliana na ajali za bararani mkoani hapa.
Chang’a ambaye alikuwa ndio dereva wa kwanza kukaguliwa alisema kuwa ili operesheni hiyo iwezo kufanyiwa polisi wanatakiwa kuanza na madereva wa malori na wale gari za IT kupima ulevi.
Alisema kuwa madereva wengi wa magari makubwa wanatabia ya kunywa pombe kila kituo hasa maeneo ya Ruaha Mbuyuni na Mikumi.
Aliongeza kuwa pombe ni kitovu cha uzembe wa ajali za barabarani. Katika hatua nyingine, Polisi mkoani Iringa wameokota mwili wa Yakobi Mhengilolo,23 mkazi wa Usokami na funding sekemara aliyekutwa amefariki dunia katika barabara ya kuelekea kijiji cha Kibengu.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa ACP Bwire alisema kuwa tukio hill lilitokea tarehe 02/07/2018 majira ya SAA 19:30hrs katika cha usokami tarafa ya Kibengu wilayani Iringa mkoani Iringa.
Alisema kuwa uchunguzi wa daktari unaonesha kuwa marehemu amevunjika shingo, mbavu mbili pamoja na kuwa na michubuko/ majeraha mwilini.
No comments:
Post a Comment