Thursday, 3 December 2015

RAS: Fufuani mifumo ya kukagua maziwa ili kulinda afya ya mlaji





Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa, (RAS) Wamoja Ayubu ametoa wito kwa wakaguzi wa maziwa kutoka mikoa ya iringa, njombe na mbeya kuwa jukumu la ukaguzi wa maziwa ni kazi yao ya msingi na sio kazi ya ziada kwao.

Alisema kuwa jukumu la ukaguzi wa maziwa kwa wakaguzi sio kazi ya ziada bali ni kazi yao ya msingi na kusisitiza watoe ushirikiano wa dhati kwa bodi ya maziwa na mradi wa uendelezaji sekta ya maziwa afrika mashariki (EADD II), ili kujenga na kuimarisa vituo vya mauzo ya maziwa.

RAS huyo alitoa rai hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya siku nne ya wakaguzi wa maziwa kutoka mikoa ya iringa, njombe na mbeya yaendelea mkoani Iringa.

Alisema kuwa kukagua maziwa ni muhimu sana kwakuendeleza tasnia ya maziwa na kulinda afya ya mlaji na hasa kwa viwanda ili kuweza kusindika maziwa wanahitaji maziwa yaliyo na viwango vya juu vya ubora.

“Napenda pia nichukue nafasi hiikuwahamasisha halmashauri zote nchini kuanzisha au kufufua mifumo ya kukagua maziwa ili kulinda afya ya mlaji,” alisema Ayubu.

Alisema kuwa katika sheria za kulinda afyaya mlaji wa maziwa nchini Tanzania zipo sheria mbalimbali kama vile sheria ya maziwa ‘The Dairy Industry Act, 2004, Tanzania food, drugs and cosmestics Act, 2003, the local government act, 1982 na ‘the public health act,1992, sheria zote hizo zina lengo kuu ka kuhakikisha maziwa yanashughuliwa kwa usafi na kumfikia mlaji yakiwa bora na salama.

lisema kuwa serikali ina jukumu la kumwahakikisha mlaji anapata maziwa bora na salama na bila ya udanganyifu kama kuchanganywa maji na pia kudanganywa kwenye vipimo.

“maziwa ni kinywaji na ni chakula muhimu katika mwili wa binadamu, kwani ni katika maziwa ndiko unapopata virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini kwa wakti mmoja. Maziwa ya protini, wanga, vitamin na madini ya aina nyingi,” alisema.

Soko la mawaziwa linashikiliwa namfumo wa soko lisilo rasmi ambalolinaaendeshwa na wachuuzi na wafanyabiashara wadogowadogo ambao huuza kati ya lita 20-100 kwa siku kutoka kwa wafugaji wadogo na mara nyingi wanatumia baiskeli kwa kusafirishia na kusambazia maziwa yakiwa ghafi.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...