MWENGE wa Uhuru utawasili Mkoani Iringa tarehe 22 Juni, 2015 na kukimbizwa hadi tarehe 26 Juni, 2015 na kuweka mawe ya msingi, utakagua, utazindua na kufungua jumla ya miradi ya maendeleo 35 yote ikiwa na thamani ya shillingi 4, 985,562,793/= .
Mkuu wa Mkoa alisema jana kuwa Mwenge wa Uhuru utapokelewa kutoka Mkoa wa Morogoro tarehe 22 Juni, 2015. Makabidhiano yatafanyika katika kijiji cha Ruaha Mbuyuni.
Akiongelea ratiba ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Iringa, Mkuu wa Mkoa alisema kuwa katika Mkoa wa Iringa Mbio za Mwenge wa Uhuru zitaanza Wilaya ya Kilolo tarehe 22 Juni 2015, Halmashauri ya Wilaya ya Iringa tarehe 23 Juni, 2015, Manispaa ya Iringa tarehe 24 Juni 2015 na Halmsahauri ya Wilaya ya Mufindi tarehe 25 June, 2015 ambapo Mwenge wa Uhuru utakuwa umekamilisha Mbio zake katika Mkoa wa Iringa.
Mkoa wa Iringa utaukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Njombe tarehe 26 June, 2015 katika eneo la Makambako kijiji cha Idofi.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa amezitaja shughuli ambazo zitafanywa na Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Iringa kuwa ni kuweka mawe ya msingi, utakagua, utazindua na kufungua jumla ya miradi ya maendeleo 35 yote ikiwa na thamani ya shillingi.4,985,562,793/= ambapo kati ya fedha hizo Serikali kuu imechangia shilingi 2,193,787,197/= Halmashauri za Wilaya na Manispaa shilingi.1,191,486,781/= michango ya wananchi shilingi1,158,299,859/= na wadau wa maendeleo shilingi 441,988,956/=.
“Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru 2015, Tumia Haki yako ya Kidemokrasia; chini ya kauli mbiu; jiandikishe na kupiga kura katika uchaguzi wa mwaka 2015”
Mwenge wa Uhuru kila mwaka hubeba ujumbe wa kudumu ambao ni:- ‘Mapambano dhidi ya Rushwa ; kata mnyororo wa rushwa chini ya kauli mbiu’’ chagua kiongozi mzalendo’’,
‘Mapambao dhidi ya dawa za kulevya; uteja wa dawa za kulevya unazuilika na kutibika chini ya kauli mbiu ’’chukua hatua’’
Mapambao dhidi ya UKIMWI; Vijana wa leo na UKIMWI chini ya kauli Mbiu ’’wazazi tuwajibike’’
Mapambano dhidi ya Maralia; Wekeza katika maisha ya baadae; chini ya kauli mbiu ’’tokomeza malaria’’
Masenza ametoa wito kwa wananchi katika Halmashauri zote za Mkoa wa Iringa kujitokeza kwa wingi kuulaki Mwenge wa Uhuru katika maeneo yote ambako utapita, kushiriki katika mikesha ya Mwenge pamoja na kupokea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu 2015.
No comments:
Post a Comment