Saturday, 2 May 2015

DK. MAHENGE AHIMIZA USAFI, UTUNZAJI MAZINGIRA NCHINI


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Dkt. Eng. Binilith Mahenge akisoma hotuba.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Dkt. Eng. Binilith Mahenge (mwenye tai ya bluu) akifurahia igizo wakati wa uzinduzi wa mradi wa mazingira wilayani Makete. Kulia kwake ni Diwani wa Iniho Jison John Mbalizi, Mkuu wa Chuo VETA-Makete Ramadhan Sebbo na Mwenyekiti wa Bodi wa CCDO Majaliwa Mayova.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Dkt. Eng. Binilith Mahenge (mwenye tai ya bluu) akikabidhi vifaa vya michezo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Wilaya ya Makete (MDFA), Bosco Godigodi Mazangalila (kulia) kwa timu za mazingira (Environmental Clubs) wanaoshuhudia ni Meneja Mradi Agnes Mahenge na Mwenyekiti wa Bodi CCDO Majaliwa Mayova


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira)  Dkt. Eng. Binilith Mahenge akionesha kitabu cha mazingira cha mwalimu cha kufundishia katika shule za msingi baada yakukizindua.




WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dkt. Eng. Binilith Mahenge (MB) ametoa wito kwa wananchi kuwa suala la usafi na utunzaji wa mazingira linaanza na mtu mmoja na hatimaye jamii nzima.

Dkt.  Mahenge alisema haya wakati wakuzindua miradi miwili ya hifadhi ya mazingira inayofadhiliwa na UNDP na Tanzania Forest Fund (TFF) kupitia Asasi ya Children Care Development Organization (CCDO) wilayani Makete, mkoani Njombe jana.

Mradi wa kwanza unaofadhiliwa na UNDP unalenga kuiwezesha jamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na mwengine unaofadhiliwa na TFF unalenga katika upandaji miti ili kuboresha hifadhi ya misitu na chanzo cha maji eneo la Unyangogo katika Kata ya Iniho.

Miradi hiyo inatekelezwa na asasi ya CCDO, inayojishughulisha na kazi ya utoaji elimu ya kupambana na mabadiliko ya tabianchi, utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji katika wilaya za Iringa na Makete.

Alisema kuwa ili kulinda afya zao wananchi hawanabudi kuyatunza mazingira kwa ajili ya vizazi vijavyo.

“Sote tumeshuhudia athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile ukame uliokidhiri, mvua zisizotabirika, mafuriko, kuongezeka kwa joto, kuibuka kwa magonjwa kama malaria katika maeneo ambayo huko nyuma hayakuwa na historia ya magonjwa hayo; mfano katika baadhi ya maeneo ya Makete,” alisema.

Alisema kuwa malaria kwa sasa imeripotiwa katika mikoa mingi ikiwemo mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya na Kilimanjaro.

“Haya yote ni ushahidi wa uwepo wa mabadiliko ya tabianchi na yanatukumbusha kwamba sote tunao wajibu wa kuhifadhi na kulinda mazingira yetu ili kuilinda nchi yetu na dunia kwa ujumla kutokana na majanga yatokanayo na uharibifu wa mazingira,” aliongeza waziri huyo.

Alisema kuwa serikali inaendelea na juhudi za kulinda na kuhifadhi rasilimali za mazingira nchini kupitia utekelezaji na usimamizi wa sera, sheria, kanuni na miongozo.

“ Nitumie fursa hii kuzielekeza mamlaka za serikali na mitaa na taasisi za serikali kutekeleza kikamilifu matakwa ya sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 kwa kuhuisha masuala ya hifadhi ya mazingira katika mipango yao ya maendeleo na bajeti zao za kila mwaka,” alisema.

Pia alitoa wito kwa asasi zisizo za serikali, taasisi za dini, na wadau wengine kushiriki kikamilifu katika juhudi za kuhifadhi mazingira na  kila mdau kwa nafasi yake.

Juma lililopita tarehe 22 Aprili, 2015, serikali ilizindua ripoti ya pili ya hali ya mazingira nchini. Ripoti hii inabainisha ongozeko la watu likiambana na kuongezeka kwa kasi kubwa ya uharibifu wa mazingira hususan misitu na vyanzo maji.

Ripoti pia imeanisha athari za mabadiliko ya tabianchi katika sekta za kiuchumu kama vile, kilimo, mifugo, uvuvi, miundombinu, wanayapori, uchukuzi, viwanda na afya.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi, Meneja wa Mradi, Agnes Mahenge alisema kuwa asasi ya children care development organization imekuwa ikijishugulisha na kazi ya kutoa elimu ya kupambana na athari za tabianchi, utunzaji wa mazingira na vyanzo maji kwa watoto na wanawake kwa lengo la kufanya watoto kuyapenda mazingira wakiwa bado wadogo na kuwa askari wema kwa nchi yao.

Pia alisema kuwa watoto kuwafanya wawe walimu wazuri kwa vizazi vijavyo hususan katika kutekelezaji wa sheria namba 20 ya mazingira ya mwaka 2004 katika kuwajengea uwezo wa uelewa, kupanua ajira na namna ya kupambana na umaskini wa kifikra na kipato.

Alisema kuwa shirika hilo limefanyikiwa kuunda timu 16  za mpira wa miguu kwa  wanaume, wanawake na watoto.

Timu hizi za mazingira ni za kudumu na lengo lake ni kuona timu hizi zinakuwa zikiendeshwa kwa mfumo wa ligi na kuwa na timu moja mama ambayo itapiganiwa kupanda daraja kwa kushiriki kwenye ligi kuu ya Vodacom huku ikifanya kazi ya kuhamasisha jamii kuhusiana na elimu ya mabadiliko tabianchi.

Wakati huohuo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mzingira) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Makete, Dkt. Eng. Binilith Mahenge alitoa vifaa vya michezo zikewemo jezi seti nne na mipra 20 kwa timu za mazingira (Environmental Clubs) kutoka halmashauri za Iringa na Makete.

Alisema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuona vijana wengi wa maeneo ya vijijini wanashirika kikamilifu katika kukuza vipaji vyao  pamoja na kutoa elimu ya uhifadhi wa mazingira.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...