Kikundi cha Singe cha vijana wakijitolea kundi Mererani 2018 wakipita mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William wakati wa mahafali ya kumaliza mafunzo ya awali ya jeshi la kujenga taifa (JKT) kikosi cha Maginga JKT wilyani Mufindi, Mkoa wa Iringa jana. (Picha na Friday Simbaya)
MUFINDI: MKUU wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri William amsema vijana wanaohitimu mafunzo ya awaliya kijeshi la jeshi la kujenga taifa (JKT) kuyatumia mafunzo wanayoyapata katika kambi mbalimbali hapa nchini kwa faida ya Taifa.
Hatua hii inaelezwa kuwa kama itazingatiwa na vijana wanaohitimu mafunzo ya muda mfupi ya JKT upo uwezekano mkubwa wa taifa kuwa na vijana ambao watakuwa waadilifu pindi watakapokuwa wakilitumikia taifa.
Akizungumza na wahitimu hao jana Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri Wiliam aliwataka kuyatumia vizuri mafunzo na maarifa waliopata katika kuliletea taifa maendeleo.
Awali, wakisoma risala yao mbele ya mgeni rasmi wahitimu hao waipongeza serikali kwa kuyarudisha mafunzo ya JKT na kusema kuwa yatasaidia katika kurudisha umoja wa kitaifa ambao kwa siku za karibuni umekuwa ukilegalega.
Akisoma risala hiyo kwa niaba ya wahitimu, Ramadhan Mohammedi akisaidiwa na Magdalena Mniko alisema kuwa mafunzo hayo ya awali ya kijeshi ya kujitolea kundi- Mererani, yalifunguliwa rasmi tarehe 22 Januari, 2018 na kamanda kikosi 514 KJ makambako kanali J.L Kashinde, ikiwa na vijana 1,185 kati yao wavulana 815 na wasichana 370.
Mohamedi alisema mpaka kufikia jana kosi imefikia wiki ya 24 ambayo ni wiki mwisho ya mafunzo hayo ya awali idadi ya kuruta 1,179 na wengine sita (6) hawakufanyiwa kuhitimu mafunzo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kushindwa uvumilivu, uvivu, kukosa ustahimilivuwa moyo na uzalendo kwa nchi yao.
Alisema kuwa katika kipindi cha cha mafunzo walijifunza stadi za maisha kama vile shughuli za kilimo, ufugaji, ujenzi pamoja na shughuli zingine za uzalishaji mali na kazi mbalimbali za kijamii.
Kwa upande wake, kaimu kamanda kikosi Kikosi cha Mafinga JKT Kapteni Victor Nkya alielezea kuwa mafunzo ya awali kwa vijana waliohitimu katika kambi hiyo kuwa yenye mafanikio makubwa kutokana na mbinu mpya zilizotumika katika kuhakikisha vijana wote waliojiunga na mafunzo hayo wanayamaliza salama.
Nkya alisema kuwa mafunzo hayo yalilenga kuwajenga ama kuwafundisha mambo mbalimbali kama vile uzalendo kwa nchi yao, upendo, umoja, mshikamano na ushirikiano, uvumilivu na ushapavu, nidhamu na ujasiriamali.
Alisema kuwa kwa ujumla wao vijana wamepikwa na wameiva na wamepata mafunzo na malezi kwa mujibu wa muongozo wa mafunzo ya kujitolea.
Jeshi la Kujenga Taifa lilianzishwa Julai 10, 1963 na serikali kwa lengo la kuwaweka pamoja vijana wa nchi hii na kuwapa malezi kuhusu uzalendo na umoja ili kuondoa dalili za matabaka zilizoanza kujitokeza katika jamii baada ya uhuru.
Baadhi ya sababu za kuanzishwa kwa JKT ni: Kubadili fikra za vijana wa nchi hii kutoka ile hali ya ukoloni kutegemea nchi nyingine kuleta maendeleo.
No comments:
Post a Comment