Wakazi wa Jimbo la Iringa Mjini wakimsikiliza kwa umakini Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu wakati wa mkutano wa hadhara wa Chadema leo uliofanyika stendi ya mabasi ya Mlandege mjini Iringa.
MNADHIMU Mkuu wa Kambi ya Upinzani ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu (CHADEMA) amezungumza na Wakazi wa Jimbo la Iringa Mjini wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Stendi ya Mlandege mjini hapa. Mbunge huyo aliwataka wakazi wa jimbo hilo kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura ili kweza kupata kadi za BVR zitakazotumika kupigia kura katika uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu.
Mbunge wa Jimbo la Iringa Mch. Peter Simon Msigwa (CHADEMA) amezungumza na wakazi wa Jimbo hilo wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika Stendi ya Mlandege mjini hapa.
No comments:
Post a Comment