Mratibu
wa Program ya Biogesi Tanzania (TDBP), Cyprian Shila (kulia) akibadilishana na mawazo na mmoja ya watendaji wa Mkoa wa Njombe baada yakumalizika kwa semina ya wakulima wa kilimo hifadhi pamoja na biogesi.
Dr.
Rehema Nchimbi(katikati), ambaye pia ni Mkuu wa Njombe akiongea na wakulima wakati wiki ya wakulima watatifi katika kilimo hifadhi na biogesi jana. Waliyeketi toka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Waging'ombe, Frederick Mwakalebela na Mkuu
wa Mradi Kilimo Hifadhi, Profesa Ndelilio Urio kutoka SUA.
Wakulima wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Dkt. Rehema Nchimbi wakati wa wiki ya wakulima mkoani Njombe.
Njombe: Mratibu wa Program ya Biogesi Tanzania (TDBP), Cyprian Shila amesema watasimika mitambo ya biogesi 4,000 kwa nchi nzima ukiwemo mkoa wa Njombe mwaka huu katika mpango wa utekelezaji kwa kushirikiana wadau mbalimbali katika sekta ya hiyo.
Shila alisema kuwa lengo la kusimika mitambo ya biogesi nchi nzima sio tu kwa kuleta maendeleo kwa wananchi tu, lakini pia kutasaidia kusafisha hewa ya ukaa ya methane (CH4) inayotokana na kuwepo wingi wa mifugo.
Hayo yalibainika wakati wa wiki ya wakulima watatifi katika mradi wa kilimo hifadhi (conservation agriculture) iliyoandaliwa na Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Programu ya Biogesi Tanzania (TDBP) iliyofanyika mkoani Njombe Ijumaa wiki iliyopita.
Alisema kuwa katika harakati za kupunguza hewa ukaa ya methane inayotokana na vinyesi vya mifugo kunakopelekea mabadiliko ya tabianchi (climate change), programu ya biogesi Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watasimika mitambo hiyo ya biogesi kwa kulima.
“ Miradi ya biogesi unatumia kinyesi cha binadamu na wanyama wanaozalisha hewa ya ukaa ya methane ambayo inachangia kuchafuzi wa hali ya hewa inayosababisha mabadiliko ya tabianchi kutaokoa pia mazingira yanayoharibika kutokana na kukata miti kwa matumizi ya nishati ya kuni na mkaa,” alisema.
Alisema ili kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana ukataji miti ovyo na kulima kilimo kisichozingatia huhifadhi, program hiyo itajenga mitambo ya biogesi pamoja kuhamasisha wananchi kutumia biogesi ilikujiletea maendeleo yao wenyewe na hatimaye kuboresha maisha kwa kupunguza umasikini.
Mratibu huyo alitoa wito kwa Watanzania kuanza kutumia nishati mbadala ya biogesi kwa kupitia kilimo hifadhi ambacho alisema ni mkombozi kwa wakulima.
Alisema matumizi ya biogesi vijijini kutasaidia kupunguza muda kwa kinamama na watoto wakike kutumia muda mwingi wa kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia.
Mkuu wa Mradi Kilimo Hifadhi, Profesa Ndelilio Urio, Makamu Mkuu wa Mradi, Dr. Peter Mtakwa na Afisa Kilimo, Alpha Mtakwa toka SUA walisema kuwa killimo hifadhi ni kilimo ambacho hupunguza matumizi ya nguvu kazi huku kikiongeza tija.
Walisema kuwa kilimo hifadhi hakihitaji mkulima kulima kwa kugatua udongo mashambani lakini kuchimba mifereji kwa ajili ya kupanda mbegu kwa kutumia mbolea ya samadi inayotokana na tope chujio (bioslurry) pamoja na mbolea za madukani.
Walisema kuwa kilimo hifadhi hupunguza muda wa kuhudumia mashamba kwa vile hutumia dawa ya kuuliwa magugu mashambani na kupunguza muda wakupalilia kwa kutumia jembe la mkono.
Walisema kuwa kwa vile udongo mwingi una upungufu wa rutuba kwa hiyo wakulima wameshauriwa kutumia mbolea mchanganyiko ili kuweza kupanda mavuno mengi.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya wakulima, Dr. Rehema Nchimbi, ambaye pia ni Mkuu wa Njombe alisema kuwa kilimo hifadhi ni mkombozi wa uharibifu wa mazingira nchini pamoja na matumizi ya biogesi, kutokana na mkoa huo kuwa na hali ya hewa inayofaa kwa kilimo.
Alisema kuwa kilimo hifadhi na tope chujio inayotokana na matumizi ya biogesi kutasaidia kurudisha rutuba katika ardhi.
Alisema mkoa wa njombe unatakiwa kuwa shamba darasa la nchi kwa kulimo hifadhi na matumizi ya biogesi kwa sababu mkoa huo hauna tatizo la migogoro ya ardhi.
Alisema kuwa migogoro mingi nchini inatokana na wafugaji wanaotangatanga na mifugo kumbe wafugaji hao wangetumia kulimo hifadhi na kuwekeza katika teknolojia ya biogesi kunawaza kupunguza migogoro mingi ya ardhi.
Awali, watafiti toka SUA, TDBP, maofisa ugani, wakulima watafiti na wadau mbalimbali walitembea shamba la utafiti Nyumbanitu Cosmas Mfugale ni mkulima wa mfano aliyepata maendeleo makubwa kwa kutumia nishati mbadala ya biogesi lililopo katika Wilaya ya Wanging’ombe, mkoani Njombe.
Kijiji hicho cha Nyumbanitu kina jumla ya wakulima watafiti nane wanaonufaika na mradi wa kilimo hifadhi ambaye pia wamejenga mitambo ya nishati mbadala ya biogesi.
Wakati huohuo, mratibu wa program ya biogesi Tanzania, Cyprian Shila atangaza kuwa maadhimisho ya siku ya biogesi kitaifa mwaka huu itafanyika tarehe 10 mwezi wa tisa mwaka huu katika mkoa wa Njombe.
Mkoa wa njombe ina jumla ya wakulima therathini ambao wanatumia kilimo hifadhi na wanatumia mitambo ya biogesi ambao walielezea faida za kilimo hifadhi na mitambo ya biogesi.
No comments:
Post a Comment