Hali tete Iringa: Inakadiriwa kuwa takribani watu 3000 wakiwemo wagonjwa wa kipindupindu wamefungiwa na Maji ya Mto Ruaha Mdogo yaliyohama mkondo wake na kutengeneza njia tofauti tatu.
Watu hao ambao wengi wao wapo vitongoji tofauti vitatu vya kilimo ya mashamba makubwa ya mpunga Tarafa ya Pawaga Iringa vijijini, hawajala chochote kwa siku pili leo kutokana na kutokuwepo kwa njia ya kuwapelekea chakula kama awali.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, Mchana huu amekiri hali hiyo na kueleza kuwa wameomba Helikopter ya Polisi kwa lengo la kwenda kudondosha chakula maeneo hayo ambayo yamegeuka kama bahari baada ya kujaa maji lakini pia kuanza kuwaokoa.
Amesema Helikopter hiyo itaondoka Dar Es Salaam muda wowote kuanzia sasa, kuja Iringa kwa kazi hiyo.
No comments:
Post a Comment