Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Usoha Njiapanda iliyopo Mbeya Vijijini.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, , Willson Mwamunyila (katikati)
akizungumza na mwandishi wa habari hizi kijijini kwake.
Baadhi ya wanakijiji wa Kijiji cha Usoha Njiapanda wakiwa katika mkutano na mwanahabari hizi.
VITISHO
na hofu ya vitendo vya ushirikina imebainika kuwa vikwanzo vya mapambano
ya baadhi ya watu wanaowatia mimba wanafunzi wa shule za msingi na
sekondari katika Kata ya Tembela Wilaya ya Mbeya Vijijini, mkoani Mbeya.
Kauli
hiyo ilitolewa juzi mjini hapa na baadhi ya wanakijiji kutoka katika
baadhi ya vijiji vya Kata ya Tembela walipofanya mahojiano kwa nyakati
tofauti na mwandishi wa habari hizi alipotembelea vijiji hivyo.
Akizungumza mkazi wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Maria Kolneri alisema
baadhi ya wazazi hushindwa kuwawajibisha watu waliowatia mimba wanafunzi
kwa kuhofia usalama wao kwani familia iliyotuhumiwa hujenga uhasama na
familia ya mwanafunzi na hata kutoa vitisho.
Alisema
katika kijiji hicho ni vigumu kwa familia ya mwanafunzi aliyetiwa mimba
kufuatilia ili sheria ichukuwe mkondo kwani huwa kuna vitisho na vingine
kutoka kwa majirani wa familia hizo. “…Hapa ukianza tu kumfuatilia mtu
aliyefanya kosa kama hilo unasikia wanakijiji wanaanza kulalamika
anataka kumfunga mwenzake sasa mtoto atakaye zaliwa atalelewa na nani…?
Watakusema huku familia yenye kosa ikitoa vitisho hadi utaacha
kufuatilia,” alisema. “Ukitaka kupata kesi (uhasama) hapa kijijini kwetu
mfunge kijana aliyempa mimba mtoto wako…, kila mwanakijiji anayekujua
atakuona hufai kwa madai kuwa umemwonea kijana uliyemshtaki,” alisema
mama huyo.
Aidha
aliongeza kuwa baadhi ya familia uhofia vitendo vya ushirikina (kulogwa)
endapo utaendelea kufutilia kesi za mimba hivyo kukata tamaa, jambo
ambalo kwa sasa kijijini hapo limekuwa la kawaida. Naye Nazareti Kibaga
mkazi wa Kijiji cha Simambwe alisema kutokana na hali hiyo wananchi
wamekuwa wagumu kufuatilia kesi za mimba jambo ambalo limefanya matukio
hayo kuendelea licha ya changamoto zingine zinazochangia uwepo wake.
“…Hali hii imefanya mimba ziendelee na hakuna kesi yoyote dhidi ya
wanaowatia mimba wanafunzi…, wazazi hawawajibiki, wananchi hawawajibiki
na viongozi nao hawawajibiki,” alisema Kibaga.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Usoha Njiapanda, Willson Mwamunyila
alikiri uwepo wa matukio ya mimba kwa kiasi kikubwa kijijini hapo
lakini alisema kikwazo katika kushughulikia matukio ya mimba ni uongozi
kukosa ushirikiano kutoka kwa wazazi na mwanafunzi. “…Matatizo ya mimba
yapo lakini wazazi na wanafunzi waliotiwa mimba hugoma kutoa ushirikiano
kwa viongozi ili wahusika washughulikiwe kisheria.
Unakuta
mtoto kapata mimba baada ya taarifa kukufikia unaenda kwa mzazi wa
mwanafunzi kuomba ushirikiano lakini wazazi wengine wanakuzunguka
wanazungumza na mwalimu kwenye shule husika na wanamalizana wenyewe,”
alisema Willson Mwamunyila. (Imeandaliwa na www.thehabari.com kwa kushirikiana na TGNP)(FS)
No comments:
Post a Comment