Hawa ni baadhi ya vikundi vya washiriki wa semina ya majadiliano ya namna ya ushiriki wa jamii katika kupinga ukatili wa kijinsia wakiwa katika tafakari leo mjini Iringa. Semina hiyo imewezeshwa na asasi isiyo ya kiserikali ya Engender-Health chini ya ufadhili wa serikali ya watu wa marekani kupitia USAID.
Mmoja ya wawezeshaji kutoka UZIKWASA- Pangani, Tanga Joseph Peniel ambaye ni programu meneja wa mawasiliano na kujenga mahusiano akiendesha semina ya majadiliano ya namna ya ushiriki wa jamii katika kupinga ukatili wa kijinsia kwa washiriki wasemina ambao ni watendaji wa kata, mtaa, wanasheria na wanaharakati.
Wawezeshaji wa UZIKWASA -Pangani Tanga Novatus Urassa ambaye pia ni Programu Meneja wa Jinsia na uongozi wenye Mabadiliko na Joseph Peniel ambaye pia ni Programu Meneja Mawasiliano na Kujenga Mahusiano kwa pamoja wakibandika karatasi zenye masuali kuhusu filamu ya AISHA, filamu hii ni kwa heshima ya wanawake wote waliowahi kubakwa na kwamba baada ya mkasa huo waliochukua hatua gani.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo wakiwa katika igizo la kusikiliza na kusikia baada ya kuangalia filamu ya AISHA. AISHA, mwanamke mfanyabiashara mwenye matamanio ya mafankio anayeishi mjini anarudi kijijini kwao kuhudhuria harusi ya mdogo wake. wakati anajikumbusha maisha yake ya zamani, na kukutana na familia yake na marafiki, kunatokea mkasa wa kubakwa wenye athari kubwa katika maisha yake. AISHA anaamua kupambana nao vikali ili kupata haki yake.
No comments:
Post a Comment