CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Iringa chaiomba serikali kuboresha mazingira na maisha ya watu wenye ulemavu nchini za kupata huduma za elimu, afya na usalama wa raia kama watu wengine.
Mwenyekiti wa CHAVITA Mkoa wa Iringa Zawadi Sumani alisema jana katika warsha ya ushawishi na utetezi kwa watendaji wa idara za serikali na viongozi wa serikali za mitaa Mkoa wa Iringa, kuwa watu wenye ulemavu ni waathirika wakubwa wa umaskini na UKIMWI hapa nchini kutokana na mitazamo potofu ya jamii inayoizunguka.
Alisema kuwa huduma na sheria mbalimbalinzilizopo hapa nchini hazikidhi maitaji ya watu wenye ulemavu na wemekuwa wakiacwa nyuma katika mchakato mzima wa maendeleo ya taifa ingawa zipo jitihada mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali katika kuhakikisha kuwa watu wenye ulemavu wanapata huduma za elimu, afya na usalama wa raia.
Lakini bado inaelekeza dhana kuwa mtu mwenye ulemavu anastahili kuishi maisha tegemezi ambapo dhana hii ina kwenda kinyume na tamko la umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu na azimio kuhusu fursa sawa na ushirikishaji wa watu wenye ulemavu la mwaka 1983.
Lengo mahususi la warsha iyo ilikuwa ni kuwapatia mwako watendaji kutoka idara mbalimbali kama polisi watendaji wa mahospitali na uongozi wa serikali za mitaa kutoka ngazi ya Mkoa hadi wilaya kutambua umuhimu wa ushiriki wao katika kufanyikisha mchakato wa uimarishaji wa sera na sheria za watu wenye ulemavu kuanzia ngazi ya mtaa, kata, tarafa hadi wilaya.
Aidha, alisema kuwa serikali hivi sasa inatekeleza awamu ya pili ya mpango wa miaka mine wa kuondoa umaskini, maarufu kama mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA, mpango huu pamoja na mambo mengine unatambua wenye ulemavu.
Warsha ya utetezi na ushawishi kwa watendaji idara mbalimbali uliaandaliwa na CHAVITA kwa kushirikiana na shirika la ‘The Foundation for Civil Society’ kwa kutoa ruzuku ambayo imefanyikisha uendashaji wa warsha ya siku nne.
Mkoa wa Iringa una kadiriwa kuwa na idadi ya walemavu wasiosikia yaani viziwi zaidi ya 2,000 wanaotabulika na chama cha viziwi Tanzania Mkoa wa Iringa.
Kwa upande wake, Mgeni Rasmi Kaimu Mkuu Mkoa wa Iringa Kapteni mstaafu Aseri Msangi, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa alisema serikali ipo bega kwa bega kuhakikisha watu wenye ulemavu hasa viziwi wanaendelea kuimarishwa kwa misingi ya kuboresha hali za maisha yao.
Alisema kuwa Chama cha tawala (CCM) kwa kuboresha ilani ya uchaguzi imeangalia mahitaji ya watu wenye ulemavu kwa kuwawekea mikakati mabalimbali ya maendeleo ya taifa, mikakati hii itasaidia sana katika kuwakomboa watu wenye ulemavu kwenye umaskini na majanga mbalimbali yanayokithiri miongoni mwa jamii ya watu wenye ulemavu hapa nchini.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa Kapteni (mstaafu) Aseri Msingi mwenye Kaunda suti ya bluu kutoka kushoto mstali wa mbele ya watu walioketi akiwa katika picha ya pamoja ya viongozi wa Chama cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) na washiriki wa warsha ya siku nne ya ushawishi na utetezi kwa watendaji wa idara za serikali na viongozi wa serikali za mitaa Mkoa wa Iringa jana. (PICHA. FRIDAY SIMBAYA)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment