MWENYIKITI wa kijiji cha Nduli, Ayubu Mwenda amedai kuwa Diwani wa kata mpya ya Nduli iliyopo Manispaa ya Iringa amekuwa akimtishia kumwondoa madarakani na pia kumnyang’anya ardhi na kuikabidhi kwa serikali ya kijiji kutokana na chuki za kisiasa.
Chuki zilizotokana na wote kuomba kuteuliwa katika kura za maoni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi ya Udiwani kwenye kata hiyo ambapo mwenyekiti huyo hakubahatika kupata nafasi na kukata rufaa ya kupinga matokeo ya kura za maoni lakini rufaa yake ilikataliwa na Idd Chonanga kupita kuwania udiwani.
Mwenda amedai kuwa vitisho hivyo alianza kuvitoa mara baada ya kupita kwenye kura za maoni pamoja na kwenye kampeni ya kujinadi kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu (Oktoba 31, 2010).
“Pamoja na kuwa kampeni meneja wa CCM wa kata ya Nduli lakini nimeonekana kuwa mpinzani kwake kwani alihisi kutokana na kushindwa kwangu ningesaidia vyama vya upinzani dhana ambayo si kweli kwa kuwa mimi ni kada wa CCM” alisema Mwenda.
Alisema mbali na yeye kupata vitisho vya kuondolewa madarakani mara baada ya kupita kwenye kinyang’anyiro cha Udiwani, diwani huyo pia alisema atahakikisha eneo analolimiliki linalokadiriwa kuwa na ekari 60 kumnyang’anya na kulikabidhi serikali ya kijiji ili lijengwe sekondari ya kata kwa lengo la kumkomesha.
“Eneo hilo lilikuwa mali ya baba yangu mzazi Abdallah Athumani Mwenda……..ambalo awali kabla ya kumiliki baba lilikuwa mashamba ya Wagiriki ambalo walikuwa akilima tumbaku na baadaye wagiriki kuondoka na kumwachia baba ambaye alikuwa akifanya kazi kwao” alisema mweyekiti huyo wa kijiji cha Nduli.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Nduli, Idd Chonanga alidai tuhuma hizo alizozitoa mwenyekiti huyo si za kweli hajawahi kusema labda ni kwa vile walikuwa wakichuana katika kura za maoni za CCM hivyo anahisi atamfanyia hivyo.
“Serikali ya kijiji ndiyo yenye mamlaka ya kumnyang’anya mkazi ardhi na kuimiliki na kuamua eneoe hilo litumike kwa shughuli zipi, hivyo mimi siwezi kumnyang’anya eneo hilo ” alisema Diwani Chonanga.
Aidha kwa upande wake Mohamed Mwenda (kaka yake Ayubu) alidai kuwa hajawahi kusikia eneo hilo kutaka kuchukuliwa na kukabidhiwa kwa serikali ya kijiji na kudai kuwa eneo hilo lenye jumla ya ekari 159 lilimilikishwa kwa mjukuu wa baba aitwae Ahamadi Mzola kwa kushirikiana na mimi (Mohamed Mwenda) kupitia wosia aliouandika Abdallah Athumani Mwenda.
Naye Afisa mtendaji wa kata ya Nduli, Hamid Mfalingundi alisema anamshangaa mwenyekiti huyo kwa kudai kunyang’anywa eneo ili lijengwe sekondari ya kata mbali na kufahamu kuwa tayari kikao kilishaamua eneo la kujenga sekondari ya kata na yeye alishiriki katika kikao hicho.
Mfalingulindi alisema makubaliano ya kujenga sekondari kwenye kikao hicho yalikuwa ni kitongoji cha Kisowele ambacho kipo kati kati ya kijiji cha Mgongo, Nduli na Kigonzile.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...
Na Friday Simbaya, Mufindi Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...
-
KIKUNDI cha Upendo ni kikundi cha kina mama 20 walioamua kujiunga kwa pamoja na kuanz...
-
Na Daniel Mbega, MaendeleoVijijini MIEMBE hulimwa karibu katika nchi zote zilizoko kwenye ukanda wa joto, na hasa tropiki. Nchini ...
-
The most deadly form of tuberculosis is one that lies in wait inside the body for years, attacking at the first sign of weakness. Abou...
No comments:
Post a Comment