Tuesday, 7 September 2010

SAIDIA MICHEZO IRINGA

Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Tagamenda Alex Kapinga mwenye koti la bluu mgongoni kuria akitoa maelekezo kwa timu yake ya wasichana ya mpira ya miguu katika mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Samora Mjini Iringa leo, kwa ajili ya maadalizi ya Kombe la Julius Kambarage Nyerere 2010.

Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake katika kombe hilo zitatoka shule za upili za Iringa Girls, Klerruu, Mawelewele, Mtwivilla, Tangamenda na Kihesa zote za Manispaa ya Iringa. Kombe la Julius Kambarage Nyerere linatarajia kufanyika tarehe 14-10-2010 kwa ajili kumuenzi Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere.

Aidha, Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira Miguu Wanawake cha Mkoa wa Iringa (IRWFA), Mwanaheri Kalolo amesema kuwa maadalizi mashindano ya kombe la Julius Kambarage Nyerere linasuwasuwa kutokana na ukata wa fedha na vitaa na pia kutojitokeza kwa wadhamini.

No comments:

ASAS AWATOA HOFU WANANCHI KUHUSU VURUGU ZA UCHAGUZI

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Salim Abri Asas , amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchagu...