Wachezaji wa Tanzania Prisons wakimdhibiti mchezaji wa Mbeya City FC, Joseph Mahundi mwenye jezi namba kumi wakati michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup 2015/16) inaendelea kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini. Mbeya City ilifungwa goli 2-1 na Tanzania Prisons katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya leo. (Picha na Friday Simbaya)
Michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup 2015/16) inaendelea wiki hii mzunguko wan ne katika hatua ya 16 bora, kwa michezo nane kuchezwa katika viwanja mbalimbali nchini.
Leo Jumamosi Februari 27, Mwadui FC imemenyana na maafande wa Rhino Rangers katika uwanja wa Mwadui Complex mjini Shinyanga wakati jijini Mbeya Tanzania Prisons wamecheza na Mbeya City kwa bamizwa bao 2-1 katika uwanja wa kumbukumbu wa Sokoine jijini hapa. Kwa mantiki hiyo Mbeya City FC imefungishwa virago na Tanzania Prison na kuaga michuano hiyo leo.
Hata hivyo mzunguko huo wa nne utakamilika kesho Jumapili ambapo Simba SC watakaribisha Singida United katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Panone FC dhidi ya Azam FC uwanja wa Ushirika mjini Moshi, huku Toto Africans wakicheza dhidi ya Geita Gold katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Bingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) ataiwakilisha Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment