Wednesday, 7 February 2018

MADIWANI WANNE WAPYA WAPISHWA MANISPAA YA IRINGA



Diwani wa Kata ya Kitwiru (kushoto)kupitia CCM anakula kiapo mbele ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Iringa katika Jimbo la Iringa Mjini huku hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa David Ngunyale (kulia) akisimamia kiapo hicho jana. (Picha na Friday Simbaya)




Diwani wa Viti Maalum Rehema Mbetwa (kushoto) anakula kiapo mbele ya Baraza la Madiwani la Manispaa ya Iringa huku hakimu mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Iringa David Ngunyale (kulia) akisimamia kiapo hicho jana. (Picha na Friday Simbaya)



MADIWANI wanne wapya wa Manispaa ya Iringa wawili kutoka CCM na wawili kutoka Chadema wameapishwa leo na kukabidhiwa nyaraka mbalimbali tayari kwa kuanza kazi ya uwakilishi wa wananchi katika maeneo yao jana. 


Walioapishwa katika baraza la madiwani ya robo ya pili ya mwaka 2018 ni pamoja na Jully Sawani kupitia CCM kata ya Kihesa ambaye katika uchaguzi wa Janauri 13 alipita bila kupingwa baada ya vyama vya upinzani kususia uchaguzi. 


Mwingine ni aliyewahi kuwa diwani wa kata ya Kitwiru Baraka Kimata ambaye Agost mwaka jana alijiuzuluwa wadhifa wake wa udiwani wa kata ya Kitwiru na kujiunga na CCM ambapo katika uchaguzi wa Novemba 26 alichaguliwa tena kuwa diwani wa kata ileile kupitia CCM. 


Madiwani wengine wawili ni waviti maalum amabo ni Maimuna Mpogole na Rehema Mbetwa wote wa Chadema, wawili hao wameteuliwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Leah Mleleu na Husna Daudi ambao walitimika Chadema na kuhamia CCM. 


Akizungumza mara baada ya kuapishwa kwa madiwani hao Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe amewataka madiwani hao kusoma vizuri kanuni za uendeshaji wa baraza la madiwani ili waweze kuwa na mchango chanya kwenye halmashauri yao. 


naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela ambaye alihudhuria kikoa cha baraza hilo la madiwani kama mshauri wa baraza hilo aliwapongeza madiwani wote walioapishwa, lakini akawaomba wakazi wa Iringa kuacha siasa za chuki alizodai kwamba hazina tija kwao na kwa taifa lao. 


Alisema vyama visiwagawe wananchi na kwamba si jambo jema kutendeana vitendo vibaya kwa kuwa hata mbinguni hakuna vyama vya siasa. 


Maidwani walioapishwa wamedai wamejipanga kuzitumikia nyazifa zao walizopatiwa na wananchi kwamba watahakikisha wanakuwa na uwakilishi chanya kwenye halmashauri yao. 


"Mimi kwanza ni washukuru wananchi walionichagua, nilikuwa diwani na nimeapishwa kuwa diwani tena safari hii ni kitokea Chama kinachoshikilia dola na ambacho ilani yake ndiyo inayotekelezwa,"alisema Baraka Kimata diwani kata ya Kitwiru. 


Diwani wa kata ya Kihesa Jully Sawani alisema yeye amejipanga kufanya kazi na asingependa kuwa mtu wa maneno maneno. 


"Mimi niwaombe wakazi wa kata ya Kihesa ushirikiano, tuachane na mambo ya siasa tufanye kazi za maendeleo, tuachane na siasa, siasa hizi za vyama zisitutangenishe sisi,"alisema Sawani. 


Madiwani wote wa viti maalumu walisema wao wanashukuru chama chao na uongozi wa Halmashauri kwa kuwaamini na kuwafanya kuwa sehemu ya baraza la madiwani na kwamba watahakikisha wanawajibika ipasavyo. 



No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...