Wednesday, 7 February 2018

MEYA MANISPAA YA IRINGA ABADILISHIWA HATI YA MASHITAKA

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Iringa imeahirisha kesi inayomkabili Meya wa Maanispaa ya Iringa Alex Kimbe ya kutishia kuua mtu kwa bastola hadi kesho baada ya mwendesha mashitaka wa upande wa Jamhuri kubadilisha hati ya mashitaka ya kesi hiyo. 


Kesi hiyo namba 189 ya mwaka 2017,ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa hoja za awali na upande wa Jamuhuri ulidai uko tayari lakini wakili wa upande wa utetezi Samson Rutebuka alidai mahakamani hapo kuwa hakuwa tayari kwa hatua hiyo kutokana na kuhitaji muda kwa ajili ya kujisoma kabla ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo.

Hakimu Mpitanjia alihoji upande wa Jamuhuri sababu za wakili wa utetezi kutopatiwa hati hiyo hadi jana ambapo alijibiwa kuwa ni kutokana na dhamira ya Jamhuri kutaka kubadilisha hati ya Mashitaka.

"Mheshimiwa Hakimu tumeshindwa kumpatia wakili wa utetezi hati ya mashitaka kwa kuwa tunatarajia kuwasilisha ombi la kubadilisha hati hiyo ,hivyo tusingempatia kabla haijasajiliwa mahakamani,'alisema Mwita.

Hakimu alikubaliana na ombi la upande wa Jamhuri na kuruhusu hati hiyo isomwe upya huku pia akikubaliana na upande wa utetezi wa kuahirisha kesi hiyo hadi kesho itakapoanza usikilizwaji wa hoja za awali.

Katika hati hiyo iliyosomwa jana na Wakili wa serikali Mwita, mahakama ilielezwa kuwa mtuhumiwa anashitakiwa kwa makosa mawili la kwanza ni la kukutwa na risasi nyingi kuliko kibali chake kinyume na kifungu namba 22 (1) a na 60 (1) cha umiliki wa siraha ya mwaka 2015.

Ilidaiwa kuwa mnamo Novemba 26 mwaka jana katika eneo la Zizi ndani ya wilaya ya Iringa mtuhumiwa alikutwa na risasi nyingi kinyume na sheria.

Katika kosa la pili ilidaiwa kuwa Novemba 26 mwaka jana katika eneo la kata ya Kitwiru wilaya ya Iringa mtuhumiwa alitishia kumuia Alfonce Patrick kinyume na sheria kifungu cha 89(2) (a ) cha Kanuni ya adhabu.

Mtuhumiwa alikana makosa yote mawili na kesi hiyo inatarajia kuaendelea kesho mahakamani hapo kwa usikilizwaji wa hoja za awali baada ya upande wa mashtaka kudai umekamilisha upelelezi.

Kimbe alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza Novemba 28, kabla ya kuahirishwa hadi Desemba 12, mwaka jana kisha kupangiwa Januari 11 mwaka huu aliahirishwa hadi Januari 29 na kisha kupangiwa February 5. 

Kesi hiyo inatarajia kuaendelea leo kwa kuanza usikilizwaji wa hoja za awali baada ya upande wa mashitaka kudai uko tayari kwa hatua hiyo na upande wa utetezi ukidai utakuwa umekamilisha zoezi la kupitia nyaraka za kesi husika. 

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...