Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA), na Halmashauri ya Manispaa
ya Iringa tumeanza zoezi la Kutambua na Kusajili wakazi wa Manispaa ya Iringa.
Zoezi
limeanza tarehe 07/06/2017 na linatarajiwa kukamilika tarehe 05/07/2017. Zoezi
linaanza saa 1 asubuhi hadi saa 11 Jioni. Zoezi litafanyika katika Vituo vya
Usajili vilivyopo katika Kata zote 18 za Manispaa ya Iringa kwa mujibu wa
Ratiba ilivyopangwa kila Kata imepangiwa siku
3 za usajili.
Zoezi za usajili litahusisha wananchi wote raia wa
Tanzania wenye umri wa miaka 18 na kuendelea.
Vitu vya Msingi anavyotakiwa kwenda navyo Mwananchi
Raia wa Tanzania katika kituo cha usajili ni:-
1. Nyaraka
halisi (original) na vivuli vya kuthibitisha uraia na umri wa Mhusika,
2. Cheti
cha Kuzaliwa,
3. Pasi ya
Kusafiria,
4. Vyeti
vya Elimu ya Msingi na Sekondari,
5. Leseni
ya Udereva,
6. Kitambulisho
cha Bima ya Afya,
7. Kitambulisho
cha Mpiga kura.
Kwa kuwa zoezi hili linahusisha upigaji wa Picha, kwa
ajili ya ubora wa picha, Tunaelekeza yafuatayo kwa wananchi:-
· kutovaa nguo Nyeupe, Kijivu, Bluu mpauko, Pinki, nguo zenye
kung’aa sana, Jezi, nguo zenye nembo, kofia aina yeyote ama kupaka Hina mikononi.
Matarajio katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ni
kusajili wakazi 130,000 kwa ajili ya Vitambulisho vya Taifa.
Mwananchi jitokeze Usajiliwe ili Upate
Kitambulisho cha Taifa kwa Maendeleo yako na Taifa kwa Ujumla
Imetolewa na:
Dennis Gondwe,
Afisa Habari- Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa
IRINGA8/6/2017
RATIBA
YA USAJILI KATIKA KATA NI KAMA IFUATAVYO:
SN
|
JINA
LA KATA
|
TAREHE
ZA USAJILI
|
1
|
KITWIRU
|
7-9/6/2017
|
2
|
RUAHA
|
7-9/6/2017
|
3
|
IGUMBILO
|
10-12/6/2017
|
4
|
MSHINDO
|
10-12/6/2017
|
5
|
KITANZINI
|
10-12/6/2017
|
6
|
MIVINJENI
|
10-12/6/2017
|
7
|
MLANDEGE
|
13-15/6/2017
|
8
|
KWAKILOSA
|
13-15/6/2017
|
9
|
ILALA
|
13-15/6/2017
|
10
|
MWANGATA
|
18-20/6/2017
|
11
|
ISAKALILO
|
18-20/6/2017
|
12
|
MKWAWA
|
21-23/6/2017
|
13
|
MAKORONGONI
|
24-26/6/2017
|
14
|
GANGILONGA
|
24-26/6/2017
|
15
|
KIHESA
|
27-29/6/2017
|
16
|
MTWIVILA
|
30/6-02/7/2017
|
17
|
MKIMBIZI
|
30/6-02/7/2017
|
18
|
NDULI
|
3-5/7/2017
|
No comments:
Post a Comment