Friday, 12 June 2015

MAHAMOD MGIMWA ANOGESHA ZAWADI ZA MSHINDI WA KOMBE LA MUUNGANO







naibu waziri wa maliasili na utalii mahamod mgimwa ambye pia mbunge wa jimbo la mufindi kasikazini.



hapa mabingwa wa kombe hilo wakishangia ushindi pamoja na mgeni rasmi pamoja na viongozi mbalimbali.



mratibu wa mashindano hayo aliyetangaza kustahafu kuratibu mashindano hayo. 




na fredy mgunda,iringa

akizungumza wakati wa kufunga mashindano ya kombe la muungano mratibu wa kombe hilo DAUDI YASSIN alimpongeza mbunge wa mufindi wa jimbo la mufindi kasikazini ambaye pia ni naibu waziri wa maliasili na utalii MAHAMOD MGIMWA kwa kisaidia kutoa zawadi.

YASSIN alisema kuwa tulipungukiwa baadhi ya zawadi kutokana na kombe hilo kufanyika bila ya kuwa na mdhamini wa kudumu hivyo aliamua kumtafuta mbunge huyo na kumuomba awasaidie baadhi ya zawadi kutokana na kukwama kwake.

"niliamua kumtafuta mbunge wetu ili atusaidie kwa kuwa tulikuwa tumepungukiwa kwenye upande wa zawadi hivyo mgunge huyo naye hakusita akatusaidia" alisema DAUDI YASSIN

baada ya hapo nilisikia minong'ono ya wananchi waliokuwepo uwanja hapo walimsifia mbunge huyo kwa kijitolea na kuwasaidia waandaaji wa mashindano hayo kutokana na waandaaji kuto kamilisha baadhi ya zawadi.

lakini wananchi hao ambao ni wapenzi wa michezo waliendelea kumuongea mbunge wao kwa kusema amekuwa akitolea mara kwa mara katika matatizo mbalimbali ya wananchi wa jimbo hilo kwa kuwa bado ana wajali na kuwapenda.


hata hivyo baadhi ya wananchi waoshabikia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) walisema kuwa licha ya wao kuwa katika chama hicho lakini bado wanaukubali na kuupokea mchango wa mbunge huyo ambaye amekuwa akisaidia maendeleo katika jimbo hilo.

niliamua kutafuta mbuge huyo kwa njia ya cm ili kujua kwanini ameamua kuwasidia wananchi wake kipindi hiki cha uchaguzi alijibu hivi "hiyo sio mara ya kwanza kufanya hivyo nimekuwa nikifanya mara kwa mara kwa lengo la kuleta maendeleo ya katika jimbo hilo"alisema mgimwa

MGIMWA aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kuendelea kumuunga mkono wakati wa kuleta maendeleo na kuacha na itikadi ya vyama,inatakiwa tukae pamoja ili tuweze kuleta maendeleo kwa kuwa akifanya pekee yake ataweza kuleta maendeleo hivyo ushirikiano kwa pamoja ndio njia sahihi ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo.



No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...