JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia mganga wa kienyeji kwa tuhuma ya mauaji ya mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa) eneo la kihesa Semtema katika Manispaa ya Iringa, mkoani Iringa.
Mganga huyo anayejulikana kwa majina ya Peter Mtuka (44) mkazi wa Sumbawanga alikamatwa na jeshi la polisi baada ya mwili wa marehmu kukutwa karibu na eneo lake lakufanyia shughuli za uganga kwa ajili ya mahojiano.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Iringa, Kamshina Msaisizi wa Polisi (ACP), John Kauga amedhitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 7:30 usiku Oktoba 26 mwaka huu.
Akielezea kutoweka kwa mtoto huyo, Kaimu kamanda alisema kuwa Oktoba 25 mwaka huu akiwa nyumbani kwao majira saa 2:30 na 3:00 asubuhi alitoweka katika mazingira ya kutatanisha, na ndipo saa 4 asubuhi wazazi wake walienda kuotoa taarifa polisi kuhusu kupotea kwa mtoto huyo katika kituo cha Polisi cha kati.
Alisema baada ya wazazi hao na majirani waliendelea kumtafuta mtoto huyo, ambapo ilipofika majira ya saa 7:30 usiku wa kuamkia Oktoba 26 walifanikiwa kumpata mtoto huyo katika moja ya pagale lililokuwa jirani na nyumba anayofanyia shughuli za kiuganga mganga huyo kienyeji akiwa amefariki dunia.
Kauga alisema baada ya kuupata mwili huo, walitoa taarifa katika kituo cha Polisi na mwili ulipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Iringa kwa uchunguzi zaidi,na ndipo vipimo vya Daktari vilisema kuwa mtoto huyo alifariki dunia baada ya kukosa hewa baada ya kukabwa na mtu au watu wasijulikana.
Aidha Kaimu kamanda huyo aliongeza kuwa mbali na kukabwa lakini pia vipimo vilionyesha mtoto huyo alibakwa na kulawitiwa na mtu au watu wasiojulikana.
Polisi walisema wanamshikilia mganga wa kienyeji kutokana na mwili wa mtoto kukutwa karibu na analofanyia shughuli za zake za uganga na kuhusianisha na tukio hilo na masuala ya ushirikina.
Naye Monica Msani ambaye ni mama wa mtoto huyo alisema kuwa anauchungu mkubwa sana kwani mtoto wake kwa mara ya mwisho alimuona akiwa anacheza na wenzie nje ya nyumba yao na ndipo alipotoka kwenda kumuangalia ili aende kunywa chai ndipo walipomkuta hayupo na wenzake kutoaelewa alielekea wapi.
No comments:
Post a Comment