Friday, 29 April 2016

WWF WAFADHILI KIJIJI CHA MBWELELI KUTEKELEZA MPANGO WA MATUMIZI BORA YA ARDHI


Afisa Maendeleo ya Jamii wa shirika la WWF, Martha Sanga akitambulisha shirika lake kwa wajumbe wa serikali ya Kijiji cha Mbweleli Kata ya Migoli, tarafa ya Isimani wilayani Iringa wakati wa kikao cha ndani jana. Shirika la WWF kwa shirikiana Halmashauri ya Wilaya ya Iringa limefadhili mpango shirikishi jamii wa matumizi bora ya ardhi wa miaka kumi (2016-2026).


Wajumbe wa serikali ya kijiji wakifuatilia kikao




Mmoja wa wajumbe serikali katika Kijiji cha Mbweleli akiwafafanulia wananchi mradi wa mpango wa matumzi bora ya ardhi pamoja na sheria namba 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka 1999 wakati wa mkutano mkuu wa hadhara uliofanyika kijijini hapo jana.

Mkazi wa Kijiji cha Mbweleli Comas Chale akiuliza swali wakati wa mkutano mkuu wa kijiji wa kutambulisha mpango shirikishi jamii wa matumizi bora ya ardhi jana, unaofadhiliwa na shirika la WWF kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.








Wataalamu kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambao ni Afisa Mipango miji na vijiji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Zahoro Mwalongo (kushoto) na Mrasimu Ramani (Cartographer) Geoffrey Mwanga wakichukua jira (points) za ardhi kwa kutumia kifaa maalum cha GPS kwa ajili ya kupima mipaka ya vitongoji vya kijiji cha Mbweleli ambavyo ni Mbweleli, Chekeckea, Quba, Sinza na Chamazala pamoja na huduma za jamii na barabara zilizopo kijijini hapo leo. Mpango umefadhiliwa na WWF na halmashauri ya wilaya ya Iringa.

No comments:

WATOTO WAITAKA SERIKALI KUTUNGA SHERIA KALI ...

Na Friday Simbaya, Mufindi  Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Mufindi mkoani Iringa wameiomba serikali kwa kush...