IRINGA: WATOTO 21 wamezaliwa katika mkesha wa Sikukuu ya Pasaka kwenye
Hospitali ya Rufaa mkoani Iringa, ambapo idadi hiyo
imeongezeka ukilinganisha na mwaka jana ambapo watoto 17 wamezaliwa wakiwemo wa
wakiume kumi na moja na wa kike sita.
Kwa mujibu wa muuguzi wa zamu, Anna Mkalimoto alisema watoto waliozaliwa hospitalini hapo kati ya hao saba ni wakiume na 14 ni wakike akiwepo mzazi mmoja aliyejifungua mapacha wa jinsi tofauti.
Akizungumza na Nipashe leo (Jumapili) kwa niaba ya Matroni, Rustica Twing’ombe, muuguzi wa za zamu huyo alisema kuwa watoto saba wamezaliwa kwa upasuaji na 14 walizaliwa kwa njia kawaida kati yao mzazi mmoja alijifungua watoto mapacha na wanaendelea vizuri.
“Watoto wote na wazazi wao wanaendelea vizuri na wengine wameruhusiwa, waliobaki wanasubiri ruhusa,” alisema.
Alisema idadi ya watoto wa kike waliozaliwa mwaka huu ni
wengi kushinda wa kiume, wakati mwaka jana watoto wakiume walizaliwa zaidi
kuliko wa kike.
Alisema kuwa mwaka jana watoto walizaliwa 17 wakiwemo wa
wakiume kumi na moja na wa kike sita, wakati
mwaka huu wamezaliwa watoto 21, wakiwemo wakike 14 na wakiume saba, sawa
na ongezeko la watoto wanne.
Alisema kuwa wakristo duniani kote wanasherehekea kufufuka
kwa Kristo kama ushindi kwa kila amwaminiye.
“Ujumbe wangu kwa wazazi wote waliojifungua kwanza na watakia
heri ya pasaka pamoja na malezi mema.,” alisema Mkalimoto.
Aliongeza kuwa katika ushuhuda wa injili anawatakia kila la
heri katika kumbukumbu ya kufufuka kwa bwana na mwokozi wa ulimwengu Yesu
Kristo kama maandiko yanavyosema.
TWENTY-ONE babies are born on the Eve of Easter at the referral
hospital in Iringa, whereas that number has increased compared to last year
where 17 children were born, including the eleven males and six females.
In accordance with the Assistance Nursing Officer on duty,
Anna Mkalimoto said babies born at the hospital, seven were males and 14 were
females and one parent gave birth to twins of the opposite sex.
Speaking to the Guardian today (Sunday) on behalf of Matron,
Rustica Twing'ombe, Assistance Nursing Officer, Mkalimoto said that seven
children were born to surgery and 14 were born through normal birth amongst them
single parent gave birth to twins and they are doing well.
"All children and their parents are doing well and others
have been allowed, but the remaining mothers are waiting for permission," She
said.
She said a number of baby girls born this year are bigger
than baby boys, but last year it was the opposite more boys than girls.
She explained that
last year 17 children were born, including the eleven males and six females,
while this year they were born 21 children, including 14 girls and seven boys, with
an increase of four children.
She said that Christians around the world are celebrating the
resurrection of Christ as a victory for everyone who believes in him.
"My message to all parents who gave birth during the
period of Easter, first and foremost I want to wish them Happy Easter and
second, I wish them also good health in
their parental care.," Said Mkalimoto.
She added that the testimony of the gospel is to wish them
all the best in memory of the resurrection of the Lord and Savior of the world,
Jesus Christ, as the Holy Bible said.
No comments:
Post a Comment